Utatuzi wa kinachoitwa sintofahamu kati ya wafanyabiashara wa soko kuu la Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi na uongozi wa Mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea umefika ukomo.
Mkuu wa Wilayani hiyo Mhe Muwango amesema kuwa mgomo huo umefikia ukomo kwa makubaliano ya kwamba tozo zote zifanyiwe mapitio ili kuondoa "tozo mzigo" kwa ajili ya kuwanusuru wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa, ili kila mmoja alipe kulingana na uwezo wake.
Mhe Muwango amemuagiza Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilayani ya Nachingwea katika kipindi cha wiki mbili kuanza mchakato wa kuanza ukarabati wa soko, kwa kuwa fedha ilitengwa katika bajeti hivyo kinachotakiwa ni utekelezaji.
Katika mkutano wa hadhara akizungumza na wananchi wakiwemo wafanyabiashara Wilayani humo Mhe Muwango amewashukuru wafanyabiashara kwa kuwa wasikivu, na hatimaye kurejesha huduma kwa kufungua maduka mara baada ya kikao hicho.
No comments:
Post a Comment