Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Madini akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Madini akisisitiza jambo kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Madini akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi.
Na Mathias Canal,
Bukombe-Geita
Halmashauri ya Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita inaongoza kwa mtandao wa barabara ambapo jumla ya kilomita
1346 zinakutikana katika mtandao huo.
Hayo
yamebainishwa leo 11 Mei 2018 na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka
Biteko (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Madini wakati akizungumza na Wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe kwenye kikao kazi kilichofanyika
katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi uliopo katika eneo la kitongoji cha
Uhamiaji, Kata ya Ketente.
Amesema kuwa Wilaya hiyo ni ya pili ikiwa nyuma ya Halmashauri
ya Wilaya ya Geita ambayo ndiyo inaongoza Mkoani Geita kwa kuwa na mtandao wa
barabara ambazo zina urefu wa kilomita 1500.
Aidha, alisisitiza kuwa tayari barabara mpya zimefunguliwa
katika kila eneo Wilayani Geita ambapo pia maombi maalumu yametumwa kwa ajili
ya kurekebisha barabara zote zinazoharibika hivyo kuwaomba wananchi kushauri na
kutunza kwa ufasaha barabara zote.
Akizungumzia kuhusu sekta ya elimu Mhe Biteko amewaeleza wajumbe
hao wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe kuwa tayari serikali imeongeza
shule za sekondari Businda kuwa na kidato cha tano na sita hivyo kuwa na shule
mbili ikiwemo shule ya Sekondari Runzewe.
Alisema kuwa ongezeko la shule hiyo litapelekea wanafunzi kupata
elimu ya ngazi ya kidato cha tano na cha sita kwa urahisi tofauti na changamoto
iliyokuwepo awali kwani wamekuwa wakitumia umbali mrefu kutafuta elimu.
Sambamba na hayo alisema kuwa jumla ya shilingi milioni 440
zinahitajika kwa ajili ya upanuzi wa mabweni ili kurahisisha huduma za malazi
kwa wanafunzi wilayani humo.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo ametafu Computer kwa ajili ya
shule hizo mbili ambapo msaada huo ameipata kutoka kampuni ya Vodacom na Wizara
ya elimu na mafunzo ya ufundi.
Kuhusu Mikopo kwa makundi mbalimbali, Wilaya ya Bukombe
inaongoza kwa kuwa nafasi ya kwanza Mkoani Geita kwa kupata fedha hizo za
mikopo jumla ya shilingi milioni 541 ambazo zimetolewa katika awamu tatu.
Mhe Biteko aliwaomba wajumbe hao wa Halmashauri kuu ya Chama Cha
Mapinduzi Wilayani Bukombe kutoendeleza makundi yaliyojitokeza wakati wa
kampeni badala yake kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili ya utekelezaji wa ilani
ya ushindi wa chama hicho ya mwaka 2015-2020.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment