Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akikagua moja ya jengo lilijengwa katika Kituo cha Afya cha Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma leo kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akikagua jengo la maabara wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa maagizo kwa uongozi wa Jiji la Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo leo, Jijini Dodoma
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Hombolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) akiongea katika ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wananchi wa Hombolo( hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma leo.
...........................................................
Na Angela Msimbira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Dodoma kukamilisha Ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo kilichopo Kata ya Hombolo Mjini Dodoma.
Mhe. Jafo ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea kituo hicho kinachojengwa kwa shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi .
Mhe. Jafo amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ni wiki kumi na sita sasa zimepita na bado kituo hakijakamilika kutokana na maamuzi ya ujenzi kuchelewa kutolewa .
“Naelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi juni, 2018 kazi iwe imekamilika na wananchi wa Hombolo waweze kupata kituo kizuri cha afya cha kuhudumia wananchi wa hapa,” anasema Jafo.
Amewataka wataalamu wa Jiji la Dodoma kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa kituo hicho ili kiendane na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Ni jukumu la wataalam kusimamia kwa uadilifu miradi ya maendeleo kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini, ni vyema kazi itakayofanyika iendane na thamani ya fedha zinazotolewa,” alisema Jafo.
Amewataka wananchi kulinda na kusimamia miundombinu ya vituo vya afya nchini vinapokamilika na kutotumia miundombinu iliyojengwa vibaya na kutegemea Serikali ndiyo yenye jukumu ya kuilinda bali miundombinu hiyo italindwa wananchi wenyewe.
Aidha ameagiza Jiji la Dodoma kuhakikisha hadi kufikia Desemba, 2018 Taasisi zote za Serikali zilizopo katika Jiji hilo zinapatiwa hati miliki kwa kuwa ndio wenye dhamana ya kutoa hati miliki katika Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment