Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akizungumza katika ukaguzi wa bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
Bweni la shule ya sekondari Endasak
Wanafunzi wa shule ya sekondari Endasak
....................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo amesikitishwa na gharama kubwa iliyotumika katika ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Endasak.
Ameyasema hayo wakati akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak leo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.
Amesema hajaridhishwa na gharama kubwa iliyotumika ya shilingi milioni 175.6 ya ujenzi wa Bweni moja wakati katika maeneo mengine fedha hizo hutumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni mawili.
"Inasikitisha sana kuona dhamani ya jengo lililojengwa haliwndani na fedha Ilizotolewana Serikali" Anasema Jafo
Amewataka viongozi w halmashauri kusimamia miaradi ya maendeleo kwa weledi na umakini mkubwa ili iendane na dhamani ya fedha zinazotolewa na Serikali.
Wakati huohuo, Mkuu wa Shule ya Endasak Mwl. Gisera Msofe amemueleza Mhe.Jafo kuwa Ujenzi wa bweni la wanafunzi wa shule hiyo umegharimu shilingi bilioni 170.6@ na mradi huo unatekelezwa kwa njia ya" Force Account"
Aidha ameishukuru Serikali kwa utoaji wa elimu bila malipo na ujenzi wa bweni kwa kuwa wanafunzi wengi wanapata elimu bila kuchangia na kuongeza hamasa kwa wazazi kusomesha watoto.
No comments:
Post a Comment