Thursday, May 10, 2018

JAFO AAGIZA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI KATIKA VITUO VYOTE VYA AFYA 208 VINAVYOBORESHWA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa agizo la ufungwaji wa mifumo ya kielektroniki katika vituo vya afya vinavyojengwa nchin.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakati alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.

.........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato katika vituo vyote vya Afya 208 vinavyoboreshwa hapa nchini.  

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo alipotembelea wilayani Chamwino mkoani Dodoma kukagua Ujenzi wa kituo cha Afya Chamwino ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amewapongeza watendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi vizuri wa miundombinu hiyo ambapo amejulishwa kuwa hadi sasa jengo la upasuaji, maabara, nyumba ya daktari, chumba cha kuhifadhi maiti, na wodi ya wazazi zipo hatua za mwisho. 

Kufuatia maendeleo hayo mazuri ya ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini, Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ili vituo hivyo vitakapokamilika viweze kukusanya mapato ipasavyo na kutoa huduma bora kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment