Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisaini vitabu vya wageni alipofika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Kilindi wakati akishiriki kutatua mgogoro wa maeneo hayo uliodumu kwa miaka 20 akiwa na Waziri wa Ardhi Mhe.William Lukuvi.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Kilindi Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemeni Jafo wakati akitoa maelekezo juu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 20.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiongea na wananchi kuhusu maelekezo ya serikali juu ya mgogoro wa Ardhi kati ya Halmashauri ya Kilindi na Kiteto Mkoani Manyara.
.............................................
Angela Msimbira OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema migogoro ikipungua katika halmashauri nchini itasaidia kupanga mipango ya maendeleo na kuongeza uchumi na kuiwezesha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa kutimiza wajibu wake.
Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi katika utatuzi wa Mgogoro wa mipaka uliodumu kwa muda wa miaka ishirini katika ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto iliyoko Mkoani Manyara na Kilindi Mkoani Tanga na kusababisha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Amesema Halmashauri zikiwa na migogoro utekelezaji wa majukumu unakuwa mgumu na kurudisha nyuma maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo hakkuna budi wananchi wakabadilika kwa kuacha migogoro na kujadili maendeleo na jinsi ya kukuza uchumi wa nchi.
“Inasikitisha kuona Halmashauri nyingi nchini zinamigogoro ambayo hurudisha nyuma maendeleo katika jamii na kuifanya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa kutoweza kutimiza malengo yake katika kuhudumia wananchi”Amesema Jafo
Mheshimiwa Jafo amesema lengo la kuja kutatua mgogoro huo uliodumu kwa miaka 20 ni kutekeleza magizo ya Serikali hivyo wananchi wanatakiwa kuwa wamoja na kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kujenga uchumi wa Nchi.
Amesema anaimani kubwa kuwa mwenendo na maelekezo katika suala zima la miradi ya maendeleo lazima litafanikiwa pale wananchi wanapokuwa katika hali ya umoja na mshikamano kwa kupunguza au kuiondoa kabisa migogoro katika jamii.
Amesema kuwa baada ya kupatiwa maelekezo ya Serikali Wananchi wa Kilindi na Kiteto wataendelea kushikamana kwa pamoja kwa kufuata maelekezo ya Serikali na kuishi kwa Amani na kufanikisha masuala ya maendeleo katika jamii zao.
Mhe Jafo amewataka wananchi wa Kilindi na Kiteto kuungana na kushirikiana pamoja ili kupunguza migogoro kwa kuwa migogoro ikiisha itasaidia kupaanga mipango ya maendeleo na kuongeza uchumi na kuiwezasha Halmashauri hizo kutekeleza majuku yao kwa ufanisi.
Aidha akiongelea kuhusu malalamiko ya wananchi wa Kibaloshi na Ilerai kuhusu kuwa na Mamlaka ya Mji mdogo Mhe. Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa kusimamia sula hilo na kuwataka wananchi kukaa vikao vya kisheria vya kujadili suala hilo ili liweze kutekezwa.
No comments:
Post a Comment