Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Asaad (kushoto)
akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean
Ndumbaro (kulia)wakifurahia jambo wakati aliokuwa kimsindikiza mara baada
Katibu Mkuu huyo kufungua mkuatano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya
CAG uliofanyika mjini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu
wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) lililofanyika mjini Dodoma leo .
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Musa Asaad
akitoa taarifa ya Ofisi yake wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi ya CAG lililofanyika leo jijini Dodoma .
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi
...........................................................................................
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),
Profesa Mussa Juma Assad amesema ofisi yake imefanikiwa kutoa taarifa kwa
wakati, kila inapofika Machi 30 ya kila mwaka licha ya kukabiliwa na changamoto
ya ufinyu wa bajeti.
Profesa Assad ameeleza hayo leo jijini Dodoma kwenye
mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambao unalenga
kupitisha bajeti ya mwaka na kujadili masuala ya kiutendaji ambayo
yanawasilishwa na kuitishwa na wajumbe.
Akizungumza katika mkutano
huo, CAG amesema ufinyu huo unaosababisha shughuli
za kiofisi kutofanyika pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya dharula
yanayoibuka nje ya ukomo wao wa bajeti.
“Baraza hii limekuwa na ufanisi mkubwa katika
kusimamia majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba,”amesema Prof.
Assad
Amesema pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo
ofisi hiyo imeyapata, bado zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili na
zinahitaji utatuzi wa kina.
Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kushindwa
kukamilisha ujenzi kwa ajili ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa kutokana na
kutotolewa kwa fedha za maendeleo kama ilivyopangwa na kwa wakati.
Aidha amesema katika utekelezaji wa bajeti ya
mwaka wa Fedha 2017/18 hadi kufikia Machi, 2018 Ofisi ilishindwa kuwajengea
uwezo watumishi kulingana na viwango vya kimataifa vya ukaguzi kutokana na
ufinyu wa bajeti.
“Kuna changamoto ya mwenendo wa upatikanaji wa
fedha za matumizi mengineyo na maendeleo kutoka mfumo mkuu wa serikali
kutoendana na mahitaji halisi ya majukumu ya Taasisi hususani ukaguzi na
mafunzo kwa watumishi,”amesema.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro ameitaka ofisi ya Taifa ya ukaguzi
kutekeleza agizo la serikali kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.
Dk. Ndumbaro amesema tayari viongozi mbalimbali
wa serikali walishahamia, hivyo ni mategemeo yake kuwa Ofisi ya Taifa ya
ukaguzi nayo pia ipo katika mkakati wa kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma
kama ambavyo taasisi nyingine zimefanya.
No comments:
Post a Comment