Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori ameyasema hayo leo wakati akisikiliza kero za wananchi wa mtaa wa Mavurunza kata ya Kimara Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Akiwa ameambatana na wataalamu wa Manispaa ya Ubungo pamoja na wataalamu kutoka DAWASCO na TARURA alianza kuwashukuru wananchi kwa kukusanyika kwa wingi katika mkutano huo na kuwataka kusema kwa uwazi changamoto zao.
Mhe. Kisare Makori amesema Ubungo licha ya uchanga wake imekuwa ikiweka mazingira mazuri kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo tumekuwa tukigusa wananchi moja kwa moja katika nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Maji, Afya, Umeme, urasimishaji wa maeneo, Utoaji wa mikopo kwa vijana na wanawake, na Miundo mbinu ya Barabara.
Nikiangalia upande wa maji kwa sasa Ubungo maji yapo changamoto ni miundo mbinu ya ulazaji wa mabomba na sasa kwa kasi ileile changamoto zitakwisha na kwa upande wa elimu Kimara haikuwa na shule ya Sekondari lakini kwa sasa tayari tumesha jenga shule ya sekondari kwa fedha za ndani na wanafunzi wameshaanza kusoma.
Lakini pia afya tumejenga sehemu ya kupumzika akinamama katika kituo cha afya cha mavurunza kata ya Kimara , na upande wa barabara TARURA wamekuwa wakijitahidi licha ya changamoto ya bajeti wamekuwa wakifanya vizuri lakini wanatakiwa kufanyakazi zaidi kuboresha miundo mbinu ya barabara katika maeneo yote ya Wilaya ya Ubungo.
"Urasimishaji tumekuwa tukirasimisha maeneo yetu kwa kuwa Wilaya ya Ubungo maeneo mengi wananchi waliwahi kujenga bila kupimwa lakini kama serikali tumeliona hilo rai yangu katika zoezi hili wako watendaji wasio waaminifu wanawalaghai wananchi kwa kuwataka kutoa kiasi kikubwa cha pesa ile waweze kurasimishiwa maeneo yao hilo ni seme tu tumetoa bei elekezi ole wao watakaoongeza bei katika zoezi hilo alisema" Makori
"Kwa Vijana na Wanawake wa Wilaya ya Ubungo tunazopesa za kutosha kuwakopesha kikubwa zaidi ni kufuata taratibu zitakazokuwezesha kuwa na sifa ya kupata mikopo hiyo na lazima pesa hizo ukikopa uweze kuzirudisha ili kuwapa fursa na wengine" Alisema Makori
"Pia niwaombe wananchi wote katika suala la ulinzi na usalama hasa vijana tukatae kwa nguvu zote mtu yeyote awe ni mwanasiasa, kikundi cha kidini, kikundi cha kijamii, hata mtu binafsi anayeonyesha dhahiri kuhamasisha uvunjifu wa amani tuliyonayo,
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amekuwa akitekeleza miradi mikubwa yenye tija kwa watanzania wote tuchukulie mfano reli ya umeme inayojengwa mradi ukikamilika mtu anauwezo wa kutumia masaa matatu tu kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma hayo ni maendeleo makubwa" Alisisitiza Makori
Mwisho Mkuu wa Wilaya amepokea changamoto na kero mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Mavurunza na kuhaidi zote zitafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo anataka wananchi wa Wilaya ya Ubungo wawe na fresh air akimaanisha mazingira bora yenye ustawi wa jamii na maendeleo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
No comments:
Post a Comment