Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza katika semina fupi ya Chama cha Polisi Wanawake.
Washiriki wa semina
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka askari wa kike wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo mkoani hapo kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na uchumi wa viwanda.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Chama cha Polisi Wanawake katika semina fupi aliyoiandaa katika Bwalo la Polisi-Dodoma kwa lengo la kuwapa Askari Polisi elimu juu ya masuala ya UJASIRIAMALI na UWEKEZAJI.
“Najua jukumu lenu la msingi ni Ulinzi wa Mali na Raia,lakini si vibaya pia mkautumia muda wenu wa ziada kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kuwaongezea kipato”amesema Mavunde
Naye,Kiongozi wa mtandao wa Askari Polisi wanawake Mkoa wa Dodoma SP Hiki amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuona haja na umuhimu wa kukutana na Askari hao na kufanikisha semina hiyo ambayo imehusisha wataalamu kutoka SIDO,Mifuko ya Uwezeshwaji na Wataalamu kutoka Manispaa ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment