Wizara ya Maliasili na Utalii
imefanya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia biashara ya utalii nchini katika Chuo
cha Taifa cha Utalii kilichopo jijini
Dar es salaam, ambapo vyombo hivyo vimejumuisha kamati ya ushauri,Mamlaka ya
rufaa pamoja na Bodi ya mamlaka ya leseni.
Akiongea leo katika uzinduzi huo Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japheth Hasunga amewapongeza wanakamati wote
waliochaguliwa na kusema kuwa anaamini kuwa watafanya kazi kwa umoja na
ushirikiano ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inapiga hatua kusonga mbele.
Pia, Naibu Waziri Hasunga amesisitiza kuwa vyombo hivyo
vya kusimamia biashara ni vyombo muhimu sana katika kuendeleza sekta ya utalii
na wajumbe wa vyombo hivyo ni muhimu kwa kusimamia sekta ya utalii nchini.
"Ni vyombo muhimu sana katika
kuendeleza sekta ya utalii na wajumbe wa vyombo hivi ni muhimu sana kwa
kusimamia sekta ya utalii hapa nchini" amesema Hasunga.
Aidha, Hasunga ameiomba Bodi ya Leseni
ya Utalii iliyochaguliwa kufanya kazi katika misingi mikuu mitatu ya utawala
bora ambayo ni Uhuru, uwazi, usawa na uzalendo ili kuepukana na migongano na
kutokuelewana nyakati za kazi.
"Nawaomba mfanye kazi katika
misingi ya utawala bora Uhuru, usawa, Haki na uzalendo"amesema Hasunga.
Katika hatua nyingiune, Naibu Waziri
Hasunga amesema kuwa sekta ya utalii ni
sekta inayochangia kiasi kikubwa pato la Taifa pia
inasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni kwa urahisi, hivyo amewaomba watanzania
kuwa wazalendo kwa kuhamasisha uhifadhi wa mazingira pamoja na utamaduni wa
mtanzania ili vivutio vizidi kuwepo kwani wasipotunza mazingira utalii
hautaendelea kuwepo.
Pia amesema kuwa japo Tanzania ina
vivutio vingi vya utalii bado mapato ni madogo ukilinganisha na vivutio
vilivyopo hivyo ameeleza mikakati ya serikali kuwa imepanga kufikia watalii
milioni mbili mpaka ifikapo mwaka 2020 ambapo jukumu hilo ni la kila Mtanzania.
"Mapato ni madogo ukilinganisha na
vivutio vilivyopo na serikali tumepanga kufikia watalii milioni mbili ifikapo
mwaka 2020 ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafikia idadi hiyo. amesema Hasunga.
Pia ameisistiza Bodi ya leseni ya
utalii kuhakikisha leseni za biashara zinatolewa kwa wakati na kwa kuzingatia
kanuni, taratibu na sheria zilizopo.
"Mhakikishe leseni zinatolewa kwa
wakati sahihi bila kucheleweshwa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria kama
inavyosema"amesema Hasunga.
No comments:
Post a Comment