Judith Ferdinand, Mwanza
Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza imebuni mikakati mipya ambayo itasaidia kuendeleza sekta ya elimu, na hatimaye kufanya na kupata matokeo mazuri katika mitihani ya taifa.
Hii ni kutokana na halmashauri hiyo kufanya vibaya na kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati amebainisha hayo juzi baada ya kumaliza kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018, kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Mwanza.
Bahati alisema wameanza kufanya mitihani ya kupima uwezo,wanafunzi kwani muda ulioisha wamefanya kiwilaya hali ambayo itasaidia kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza kimkoa kama ilivyokua mwaka 2015,
Alisema wameondokana na utaratibu wa kila shule kufanya mitihani yake ya muhula,hivyo muhula ulioisha wamefanya ya pamoja kama wilaya ambayo haina tofauti na taifa.
Pia alisema, mitihani hiyo imechapwa na Halmashauri,kugawiwa pamoja na kusimamiwa kwa mfumo wa taifa,ili kuweka uwiano na usawa wa kupata wahitimu ambao wanaendana na mazingira halisi ya mtihani wa taifa.
“Tumeondokana na utaratibu wa kila shule kufanya mitihani yake ya mhula, kwani muhula uliyoisha tumefanya ya pamoja kama wilaya ambayo hainatofauti na yataifa, na imechapishwa na halmashauri, sambamba na kugawiwa na kusimamiwa kwa mfumo wa taifa,ili kuweka uwiano na usawa wa kupata wahitimu ambao watakuwa na uwezo na kunaendana na mazingira halisi ya mtihani wa taifa, tofauti na zamania ambapo unaweza kuwa na wanafunzi ambao wamefaulu vizuri kwenye mitihani ya mhula na taifa kufanya vibaya,” alisema Bahati.
No comments:
Post a Comment