Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya
Mwanamke na Uongozi akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na
Taasisi ya Vijana ya TYVA
uliolenga
kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency
Park Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vijana kutoka sehemu
mbalimbali za Jijini wakifuatilia mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya
Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika
kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika
hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
Bw. Oscar Munga akichangia hoja wakati
wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa
na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga
kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency
Park Jijini Dar es Salaam.
Bi. Anna Winstone akichangia hoja
wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa
na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga
kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency
Park Jijini Dar es Salaam.
1.
Mmoja wa washiriki wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na
Taasisi ya Vijana ya TYVA
uliolenga
kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency
Park Jijini Dar es Salaam.
Na
Mwandishi Wetu, Dar es salaam
VIJANA nchini wametakiwa kutambua wajibu wao katika Taifa kwa
kutumia fursa zinazojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi katika
jamii ili kutetea maslahi na agenda mbalimbali zinazogusa maendeleo yao.
Hayo yamesemwa leo Jumamosi (Desemba 17, 2017) Jijini Dar es
Salaam na Mkuu wa Ushawisihi na Utetezi wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, Yusuf
Bwango wakati wa mdhahalo wa vijana uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia
mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Kwa mujibu wa Bwango alisema tafii mbalimbali zimebaini kuwa
Vijana wengi wamekuwa na mtazamo hasi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za
Uongozi hususani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kubaki nyuma katika nafasi
hizo huwaniwa na kushindaniwa na Wazee pekee.
“Tumefanya mdahalo huu kwa malengo ya kuwajengea uwezo vijana
kutambua kuwa wao ndio Viongozi wa baadae na hili litaanzia katika chaguzi
mbalimbali zinazofanyika katika ngazi za kijamii ikiwemo chaguzi za Serikali za
Mitaa” alisema Bwango.
Bwango alisema umefika wakati kwa Vijana wa Kitanzania kuweza
kutumia majukwaa mbalimbali ili kuweza kubadili fikra na mitazamo yao kuhusu
mifumo ya kiutawala na kutumia majukwaa hayo kuunda vyombo imara vitakavyoweza
kuwasilisha na kupaza sauti zao.
Aliongeza kuwa mdahalo huo pia umekusudia kuwawezesha vijana
kupata taarifa mbalimbali kuhusu nafasi ya vijana kitaifa na kimataifa pamoja
na juhudi mbalimbali zilizochuliwa na Serikali kuwasaidia vijana kuweka kupaza
sauti zao ikiwemo uanzishaji wa vyombo maalum vya utetezi wa Vijana ikiwemo
Mabaraza ya Vijana.
Akifafanua zaidi Bwango alisema kupitia mitandao hiyo Vijana
wataweza pia kuwasiliana na kuunganisha nguvu ya pamoja itakayowezesha kujadili
changamoto na mikakati mbalimbali itakayowawezesha kuwaletea maendeleo yao
kupitia Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Alisema tangu Mwezi Julai hadi Novemba, mwaka huu TYVA imeweza
kutoa elimu ya uraia kwa vijana wa Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dodoma, Dar
es Salaam,, Morogoro, Tanga, Pwani, Zanzibar na kuwawezesha vijana kutambua
wajibu, nafasi na haki za kikatiba waliyonayo katika Taifa.
Bwango alisema katika midahalo hiyo iliyoendeshwa na TYVA kwa
kushirikana na Mamlaka mbalimbali za Serikali, vijana wengi waliweza kupatiwa
elimu ya uraia pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua kiuchumi
ikiwemo elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Kwa upande wake, Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke
na Uongozi alisema mapambano ya harakati za ukombozi katika jamii hususani kwa
wanawake zitafanikiwa kwa kujenga mkakati wa pamoja wa ushawishi utakaoweza
kuondoa vikwazo mbalimbali vilivvyopo kaika mfumo ya kiutawala.
“Ili kujikwamua na kufikia na juu katika ngazi za maamuzi ni
wajibu wa wanawake wote kuunda mkakati wa pamoja na kuacha kusubiri na tufute
dhana ya mwanamke ni kiumbe dhaifu” alisema Sumaiya.
MWISHO
No comments:
Post a Comment