Serikali
kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameipa Menejimenti
ya Makumbusho ya Taifa muda usiozidi miezi miwili iwe ishabuni vyanzo vipya vya
mapato ili iweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili baadala ya kutegemea ruzuku
pekee kutoka serikalini.
Amesema
Makumbusho ya Taifa ina mali nyingi lakini imekuwa hajui namna ya kuzitumia ‘’Mkae
chini mnambie namna gani mnaweza kuongeza mapato katika rasilimali mlizo nazo halafu mniletee andiko ofisini kwangu ndani ya muda usiozidi miezi
miwili ’’ Aliagiza
Amesema
kazi kubwa ya Makumbusho ya taifa ni kuhifadhi lakini wakati ikihifadhi
inahitaji kupata mapato kidogo hapo hapo ili iweze kuendelea kuwepo.
Aliyasema
hayo leo
alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Makumbusho ya Taifa makao Makuu
jijini Dares Salaam wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujionea namna
Taasisi hiyo inavyofanya kazi
,Aliwataka Watumishi
hao wasitumie muda mwingi kulalamika
baadala yake wasaidie katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ili viwasaidie katika
kujikwamua kimapato.
Naibu
Waziri Hasunga aliongeza kuwa, licha ya Serikali ya kutambua umuhimu wa Makumbusho hayo lakini
hata hivyo Serikali imekuwa na masuala mengi yakufanya na yanayohitaji pesa
katika kuyashughulikia.
Wakati huo
huo, Ameiagiza taasisi hiyo ijitangaze kwa vile imekuwa haijulikani licha
ya kuwa na umuhimu mkubwa katika
kuihudumia jamii.
‘’Mmekuwa
mnafanya mambo makubwa kisiri kisiri kwa
ajili ya wananchi lakini wananchi mnaowahudumia hawajui mnayoyafanya kwa ajili
yao hivyo jitangazeni’’ alisisitiza.
Pia, Aliwaagiza
watumishi kuendelea kufanya tafiti ili waweze kuvumbua mambo mengi zaidi
yatakayoisadia Taasisi hiyo kuweza kupiga hatua katika kuihudumia jamii.
‘’Sisi kama
serikali hatujaweza kufanya vizuri katika eneo la utafiti tumekuwa tukitenga bajeti ndogo lakini kwa kulitambua
hilo nataka mpate pesa ya kutosha ili mfanye tafiti nyingi zaidi’’ alisisitiza
Aidha, Ameiagiza
Menejimenti hiyo iimarishe mfumo wa ndani katika masuala ya Tehama, alisema
haiwezekani taasisi hiyo hadi hivi sasa isiwe na kanzidata licha ya changamoto
kubwa ya udukuzi unafanywa na mataifa makubwa katika masuala ya uhifadhi.
Awali, Mkurugenzi Mkuu, Prof. Fortunatus
Mabula amemuhakikishia Naibu Waziri Hasunga ushirikiano mkubwa katika kazi.
Aidha, Prof.
Mabula alimwambia Naibu Waziri kuwa
tayari wameshapata eneo la kujenga makumbusho ya Marais katika eneo la
Iyombe mjini Dodoma ikiwa ni kutekeleza
agizo alilolitoa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla alipozungumza na wadau wa Wizara mwezi
uliopita mjini Dodoma
MWISHO
No comments:
Post a Comment