Wanaharakati wa kata ya kipunguni wakicheza kwa pamoja na watoto wa kata hiyo mara baada ya kuwapa elimu juu ya kupinga ukeketaji na rushwa ya ngono mapema jana jijini Dar es salaam. |
Wanaharakati wa kata ya Kipunguni wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana jijini Dar es salaam. |
Na Vicent Macha
Kituo cha sauti jamii Kipunguni jana tarehe 29 mwezi desemba kimezindua kampeni mahususi ya kutoa elimu mtaa kwa mtaa, iliyofuatiwa na zoezi kugawa vipeperushi pamoja na kubandika karatasi zenye jumbe mbalimbali katika kata hiyo.
Akiongoza kampeni
hiyo Mkurugenzi wa Sauti jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi alisema kuwa lengo
kuu la kampeni hiyo kuangazia sehemu kuu mbili ambazo ni kupinga ukeketaji
katika kata hiyo lakini pia rushwa ya ngono katika jamii ya kitanzania.
Aidha Bw. Bishagazi
alidai kuwa kampeni hiyo imelenga kupinga vitendo vya ukeketaji ambavyo
vinavyotarajiwa kutekelezwa mwakani 2018 kwani ndio mwaka mahususi kwa kukeketa
hususani kwa makabila yanayotokea mkoani mara ambayo yameshamili katika kata
hiyo.
Aliendelea kusema
kuwa watekelezaji wakuu wa mambo haya ni watu tunaoishi nao katika jamii zetu
na kesi zake zinakuwa ngumu kusikilizwa kutokana kwamba watekelezaji wa hayo ni
baba, mama au shangazi hivyo inaleta ugumu katika kutoa ushahidi na mtoto anaogopa
kwa kuwa anajua mzazi wake au ndugu yake atafungwa kwa sababu yake.
“Wanaharakati
wengi wamekuwa wakisubiri zoezi la kukeketa lianze ndipo waanze kuwakamata wahusika
wakiwa tayari wameshakeketa, lakini kwetu sisi tumeona tuzuie kabla watoto hawa
hawajafanyiwa ukeketaji ili kuweza kuwakomboa juu ya mila na tamaduni mbaya
kama hizi” alisema bishagazi
“Kampeni hii
itakuwa ni endelevu lakini pia tutajaribu kuwa karibu na wananchi ili waweze
kutupa taarifa mbalimbali kuhusu wakeketaji na tutakaa nao chini tutajaribu
kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili waachane na mambo hayo ya kizamani
na mila potofu ya kukeketa na waweze kuwa watu wema katika jamii”. Alisema Mkurugenzi
huyo
Lakini pia
katika maeneo mengi hususani maeneo ya kazi, vyuoni, mashuleni maeneo ya
biashara wananchi wanalazimishwa sana kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupata
huduma stahiki wanayohitaji, ndio maana sauti jamii kipunguni imeamua kuanzisha
kampeni hii ya kupinga rushwa ya ngono katika jamii zetu.
Sauti jamii
kipunguni kwa kushrikiana na mashirika rafiki kama Global Fund na TGNP na
mengineyo tutawezeza kutoa elimu kwa wananchi na kuwawajibisha waajili,
madaktari, walimu na watu wote walio katika sekta za Umma na binafsi ili waweze
kupinga na kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo wataombwa rushwa ya ngono
watu hao.
ANGALIA VIDEO HII KUJUA KILICHOENDELA ZAIDI...
No comments:
Post a Comment