Mkurugenzi Mtendaji wa Reaching Out Destinies Foundation(RDF) Bi. Jane David akifungua rasmi kwa maombi sherehe za kuwashukuru wadau wao kwa kuwa nao kwa muda wa mwaka mzima, na baadae kutoa shukurani zake za dhati kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema akielezea historia ya asasi hiyo,kuwa walianza wakiwa wa 3 lakini kwa sasa wapo zaidi ya 1300,na kwa mwaka huu walifanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh milioni 1o ambazo zimeweza kuwasaidia watu wenye makundi maalum wakiwemo yatima na wajane.
Mkurugenzi wa Miradi ya nje na Mahusiano kutoka (RDF) Bi. Jackline Nicetas akielezea namna asasi yao inavyofanya kazi pia kuwafikia watu mbalimbali wenye uhitaji hasa wale waliopo majumbani, ambapo waliweza kuwaona wajane 3 mkoani Dar es salaam na Mjane mmoja mkoani Pwani, pia wameweza endesha semina,kuwa na camp na mentor ship forum
Bi Josephine Mbago akitoa shukurani zake za dhati kwa RDF kwa kwenda mpaka mkoani Pwani kumuona Mama yeke ambaye sasa ni Marehemu na kuwasaidia kwa kile walichokuwa nacho, na kusema kuwa alijifunza kuwa 'hautakiwi kuwa na elimu wala pesa ndio uweze kumasidia mtu bali talanta uliyokuwa nayo ndio itakuwa msaada mkubwa kwa wengine', mwisho aliwaombea kwa Mungu awazidishie zaidi pale palipo pungua.
Mwanadada Pili Amani ambaye pia ni Mwimbaji akitoa ushuhuda wake namna RDF ilivyo msaidia ambapo alisema kuwa unapompa mtu pesa bila kumpa moyo haimsaidii, aliwashukuru sana kwa mambo waliyo mtendea na kuwaombea waendelee kuwa na moyo huo. Alimalizia kwa kusema kuwa kumpenda mtu ambaye haujawahi kuonana nae ni jambo la muhimu na Mungu anakubariki.
Mwanachama wa RDF Bi. Frida Bariki akishukuru kwa yeye kukutanishwa na RDF ambapo alisema kwake ulikuwa ni ushuhuda mkubwa ambapo amejifunza upendo,moyo mkunjufu na kujitoa pia aliwaombea Mungu awape moyo wa unyenyekevu na awape uwezo wa kutenda mambo makubwa zaidi
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Ambrose Wankamba akitoa pongezi na shukurani kwa asasi ya RDF kwa kuwatembelea ambapo waliweza kuwabadilisha katika mambo mengi sana na kuwaomba wapate kuwatembelea tena pindi watakapo pata nafasi.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Bi. Lightness Mamkue akitoa shukurani zake za dhati kwa niaba ya shule yake kwa RDF ambapo wamewafanyia mambo makubwa ambayo kwa moyo wa binadamu hawawezi kuyaona lakini rohoni, ambapo pamoja na wao kuanza kuwalea wanafunzi kiroho zaidi.
Afisa Elimu Kata ya Mzinga , katika Manispaa ya Ilala Bi. Yusta Grant alisisitiza kuwa pamoja na kuwasaidia watu kifedha au kwa vitu mbalimbali pia ni muhimu kuongea nao na kuwapa moyo kama RDF wafanyavyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mzinga, Manispaa ya Ilala Bw. Geral Salota akitoa salam zake za Shukurani kwa RDF na kuahidi kuendelea kuwaombea kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Bi. Saum Rashid kutoka Ulingo/Jumuia ya Wanawake , akitoa shukurani zake za dhati kwa RDF kwa kuendelea kufanya vizuri katika kazi zao za kuwasaidia wale wenye mahitaji na kuwasihi waendelee hivyo hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji (RDF) Bi. Jane David (kushoto) na
Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema (kulia) pamoja na wageni wengine (hawapo pichani) wakimuombea muongozaji wa kipindi cha Jukwaa la mazungumzo kinachoitwa 'Destinies Series' Bi.Jackline Nicetas (wa kati kati) kabla ya kipindi hakijaanza.
Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema (kulia) pamoja na wageni wengine (hawapo pichani) wakimuombea muongozaji wa kipindi cha Jukwaa la mazungumzo kinachoitwa 'Destinies Series' Bi.Jackline Nicetas (wa kati kati) kabla ya kipindi hakijaanza.
Mgeni Rasmi katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa RDF na ufunguzi wa Jukwaa la mazunguzo la 'Destinies Series' Mchungaji Salome akizungumza mambo mbalimbali ambapo baadhi ya mambo aliyoongelea ni pamoja na kushindwa kujiandaa ama kusimamia vipaumbele vyako sahihi vinaweza kuathiri hatma ya maisha yako.
'Talk Show' ikiendelea
Mwongozaji wa kipindi hicho Bi. Jackline Nicetas akiendelea kuchokoza mambo mbalimbali
Maombi mbalimbali yakiendelea
Wageni wakiwa wanasikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kutimiza mwaka mmoja wa RDF
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje
No comments:
Post a Comment