Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) alipotembelea mamlaka hiyo mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye picha ya pa moja na menejimenti ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) alipotembelea mamlaka hiyo mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mbele kulia) akiwa na Msimamizi wa Mradi, Mhandisi Richard Magwizi (kulia) wakipita kwenye moja sehemu ya mradi wa Same-Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso
amezitaka taasisi za Serikali kulipa madeni ya ankara za maji kwa mamlaka za
maji nchi nzima, ili ziweze kutoa huduma bora ya maji inayokidhi mahitaji ya
wananchi.
Aweso alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na
watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA),
alipotembelea mamlaka hiyo kwa dhumuni la kujionea utendaji wa mamlaka hiyo
mkoani Kilimanjaro.
‘‘Mamlaka za Maji nchini zimeendelea kukabiliwa na
changamoto ya malimbikizi makubwa ya madeni ya ankara za matumizi ya maji kwa
taasisi za Serikali, ambazo zimekuwa zikipata huduma ya maji na kushindwa kulipa kwa wakati,
ambapo hadi kufikia Machi 2017 deni lilikuwa limefika Sh. bilioni 39.94’’,
alisema Naibu Waziri.
Aweso alisema wizara itaangalia jinsi ya kufanikisha ulipwaji
wa madeni hayo, ili kuimarisha huduma ya maji mijini kufikia asilimia 86 mwezi
Juni, 2017 na 95 ifikapo mwaka 2020 kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha, Naibu Waziri Aweso ametembelea mradi wa maji wa
Same-Mwanga ambao unatekelezwa katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro kwa
nia ya kuhakikisha unatekelezwa vya ubora na kukamilika kwa wakati.
Mradi huo mkubwa unategemea kuhudumia zaidi wa watu
400,000 wa vijiji 38 katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe, unatarajiwa
kugharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 300 na kukamilika Mei, 2019.
MWISHO
No comments:
Post a Comment