Waziri wa mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi akizindua kampeni za chama cha mapinduzi CCM katika jimbo la Longido miongoni mwa matatu yanayowaniwa kwenye uchaguzi mdogo wa Januari 13, 2018 amesema sababu iliyowafanya vyama sita vya upinzani kuususia uchaguzi ni hofu ya kuambulia patupu.
Mwigulu amesema viongozi hao waliotangaza majuma kadhaa yaliyopita kutoshiriki uchaguzi huo wanahofia baada ya kupima uitikio wa wananchi kwa serikali na wanaikubali kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye anaitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo na inaonekana.
Yafaa kukumbukwa kuwa katika uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi novemba mwaka 2017 uliokuwa ukijumuisha kata 43 upinzani uliambulia kata moja pekee huku Chama tawala kikishinda kwa kishindo katika kata 42.
Akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi huo Dr. Steven Kiruswa, Waziri Mwigulu amewasihi kumchagua kwani chama kimejihakikishia atatekeleza vyema ilani ya uchaguzi na kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Longido ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.
Comrade Mwigulu vilevile amewahakikishia wananchi usalama katika siku ya uchaguzi na hivyo kuwataka kutumia vyema haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi huo mdogo.
Mwigulu akizungumza na wananchi na wanachama waliohudhuria ufunguzi wa kampeni katika jimbo la Longido hivi leo.
baadhi ya wananchi waliopata kuhudhuria mkutano huo wa kampeni.

No comments:
Post a Comment