Mtoto Lucia
Thomas Mwenye umri wa miaka 12 amekutwa akiwa ameuawa na mwili wake kutupwa
eneo la makaburi mtaa wa mkoani mjini Geita.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mkoani, Salvatory Edward amedai pamoja na kunyongwa hadi kufa, mwili
wa mtoto huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi
Kiandege wilayani Bunda pia ulikuwa na dalili za kubakwa kabla ya kuuawa.
Mama Mkubwa wa mtoto huyo Bi, Grace Thomas amesema hata wao wameshangazwa na tukio hilo kwani
mtoto huyo alikuja Geita akitokea Jijini Mwanza akiwa salama na kwamba kwa mtut
ambaye ametenda ukatili huo ni vyema kwa
vyombo vya sheria vikafuatilia kwa umakini hili waweze kumchukulia hatua za
kisheria.
Mama Mzazi
wa Mtoto huyo Bi, Mary Thomas alisema mwanaye alitoka nyumbani jana Alhamisi
saa 12:30 jioni akiwa ameongoza na mtu aliyesema ni mwalimu wake wa masomo ya
maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa maelezo kuwa anaenda kuchukua
karatasi za mitihani ya somo la Uraia.
Aidha ameongeza
kuwa baada ya kuona usiku umeingia bila mtoto kurejea nyumbani, alikwenda kwa
mwalimu mwingine aliyemtaja kwa jina moja la ambapo waliongoza hadi nyumbani
kwa mwalimu aliyeondoka na mwanaye na kumkuta lakini akawatoroka kwa kujifanya
anampa mtu begi alilolishika mkononi.
Baada ya
mwalimu huyo kutorejea huku mtoto haonekani, waliendelea kumtafuta mtoto wake
usiku kucha bila mafanikio ndipo alipoenda kutoa taarifa polisi alikotakiwa
kurejea iwapo itapita saa 24 bila mtoto kurejea nyumbani.
“Kabla ya
saa 24 kumalizika, taarifa zilinifikia kuwa mwili wa mwanangu umeonekana
makaburini akiwa tayari amefariki huku ukiwa na michubuko shingoni na akiwa
amefungwa kamba miguuni huku hana nguo ya ndani,” Bi,Mary alisema kwa uchungu.
Kutokana na
tukio hilo, uongozi wa serikali ya mtaa wa mkoani umepiga marufuku vituo vyote
vya masomo ya ziada eneo hilo na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto
wao kwenye shule zinazotambulika kisheria badala ya vituo vya vichochoroni.
No comments:
Post a Comment