Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Jinsi uzalishaji wa Chai unavyohifadhiwa wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha Itona kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo, Jana Disemba 5, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba ya Chai Kijijini Itona, Kata ya Ifwagi wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha Itona kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo, Jana Disemba 5, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wakulima wa zao la Chai katika Kijiji cha Itona, Kata ya Ifwagi, Wilaya ya Mufindi wakati wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa . Jana Disemba 5, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Jinsi zao la Pareto linavyochakatwa kiwandani wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchakata Pareto cha PCT cha Mjini Mafinga wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa. Jana Disemba 5, 2017.
Na Mathias
Canal, Iringa
Wamiliki wa viwanda nchini wametakiwa kutoa ajira
za uhakika/mkataba kwa wafanyakazi wao ili kuongeza ufanisi wa ajira kwani
asilimia kubwa ya viwanda nchini vinaajiri wafanyakazi kama vibarua jambo
ambalo linaweka mashakani ajira zao.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai
cha Itona kilichopo Wilayani Mufindi
Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo.
Mhe Mwanjelwa Alisema kuwa kutoa ajira zisizo na
mikataba/vibarua ni sehemu ya kuwazalilisha wananchi hususani watanzania kwani
wanasalia kufanya kazi kubwa huku wakiishi kwa hofu badala yake ajira hizo za
mikataba zinaweza kuendelea kwa wageni na sio wazawa.
Mbele ya Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini
Itona, Kata ya Ifwagi Wilayani Mufindi Mhe Mwanjelwa aliwahakikishia wakulima
kuboreshwa soko la zao hilo kwa kutangaza bei elekezi ya serikali hivi karibuni
ili kupunguza unyonyaji unaofanywa na wamiliki wa viwanda kwa kununua malighafi
hizo kwa bei ya chini ambayo kwa kiasi kikubwa haiwanufaishi wakulima.
Aliwataka wamiliki wa kiwanda cha Kusindika na
Kuchaka Chai cha Itona kuongeza nguvu
katika ununuzi wa Chai kwa wakulima kwani asilimia 21 ya chai wanazonunua kwa
wakulima wote wa zao hilo ni chache ukilinganisha na uzalishaji wao mkubwa.
Alisema wanapaswa kuongeza tija katika ununuzi
angalau kufikia asilimia 40 ili kuwaongezea soko wakulima hao jambo
litakalowanufaisha ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji ukilinganisha na
uzalishaji mdogo wa sasa.
Sambamba na hayo pia aliwataka kuanzisha mashamba
darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la chai kwa wakulima hao
ili waweze kuwa na uzalishaji bora katika zao hilo.
Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa aliwapongeza
wamiliki wa kiwanda hicho cha kusindika na kuchakata chai cha Itona kwa idadi
kubwa ya kuajiri wazawa ambapo zaidi ya watanzania 1500 wameajiriwa huku wageni
wakiwa wanne pekee.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa amehitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa ambapo
alitembelea pia kiwanda cha kuchakata Pareto cha PCT cha Mjini Mafinga na
kukagua maabara ya kupima ubora wa Pareto sambamba na kuzungumza na uongozi wa
kiwanda hicho ili kuboresha na kuongeza bei ya ununuzi wa zao hilo kwa
wakulima.
MWISHO
No comments:
Post a Comment