Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde ameyataka makampuni,viwanda na Taasisi mbalimbali nchini kusaidia kufadhili mchezo wa Karate nchini ambao umeanza kukua kwa kasi hivi sasa.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua mashindano ya kitaifa ya Karate katika ukumbi wa Kilimani Dodoma yanayojumuisha Timu za Karate kutoka Mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya timu waalikwa kutoka Kenya.
“Wafadhili wengi hivi sasa wameweka nguvi kubwa katika kusaidia michezo ya mpira miguu,pete,wavu na kikapu,ni muda sasa muafaka sasa kuangalia aina mingine ya michezo kama huu wa karate ambao unaweza kutuletea sifa katika medani za kimataifa”Amesema Mavunde.
Awali, akimkaribisha Mavunde, Kiongozi wa Karate nchini Kitte Mfilinge amemuomba Waziri Mavunde kusaidia kuutangaza na kuukuza mchezo huu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili upate uzito unaostahili kama ilivyo michezo mingine.
No comments:
Post a Comment