Judith Ferdinand, Mwanza
Inaelezwa kwamba uwekezaji katika rasilimali watu unawezesha kukuza uchumi wa taifa kukua kwa kasi hivyo vyuo vya elimu ya juu vimeaswa kuzalisha wasomo bora ili kutimiza vyema lengo hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM), Profesa Lettice Rutashobya aliyasema hayo wenye Mahafali ya nne ya chuo hicho tawi la Mwanza, yaliyofanyika juzi chuoni hapo jijini Mwanza.
Profesa Rutashobya alisema kukua kwa uchumi wa nchi yetu kunategemea ni kiwango gani tumewekeza kwenye sekta ya elimu,hivyo ni jukumu la vyuo vya elimu ya juu nchini ikiwemo IFM kutekeleza jambo hilo.
Hivyo aliwataka wahitimu kuelewa kuwa elimu walioipata ni mwanzo wa safari ya kupata elimu ya juu hasa wakizingatia kukua kwa utandawazi na mahitaji ya ajira.
Aidha aliongeza kuwa wahitimu ni vizuri wakajua kwamba ni wajibu wao kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabili mabadiliko yatokanayo na utandawazi sambamba na kuwa waaminifu na waadilifu katika kusinamia fedha za waajiri wao.
No comments:
Post a Comment