Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Singida Vijijini, Grace Shindika (wa tatu) pamoja na wahitimu wengine wakitunukiwa Shahada ya Uzamili (Masters) ya Utawala katika Elimu ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT Jijini Mwanza, hii leo Jumamosi Disemba 09,2017.
Shindika amekuwa miongoni mwa wahitimu 2124 waliohitimu ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada mbalimbali katika mahafali hayo ya 19 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT mwaka huu 2017 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Jude Thadeus Ruwaich ambaye amewataka wahitimu hao kutumia vyema elimu waliyoipata katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo nchini na hivyo kukuza kukuza uchumi wa Taifa kupitia Tanzania ya Viwanda.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dr.Thadeus Mkamwa amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya wanafunzi kushindwa kupata elimu ya Chuo Kikuu nchini kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada hivyo mamlaka zinazohusika na mikopo kwa wanafunzi ni vyema zikaendelea kuboresha upatikanaji wa mikopo ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kupata elimu.
Katika Mahafali hayo, wahitimu 424 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na changamoto mbalimbali huku baadhi ya waliofanikiwa kuhitimu masomo yao wakibainisha kwamba watatumia vyema elimu waliyoipata kwa kuhakikisha azima ya Tanzania ya Viwanda inatimia kwa wao kutengeneza mazingira bora ya kujiajiri.
No comments:
Post a Comment