Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Naibu Waziri OR TAMISEMI, Joeseph
George Kakunda baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi na
Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika mjini
Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Naibu Waziri OR TAMISEMI, Josephat
Sinkamba Kandege baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi
na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika
mjini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mawaziri OR TAMISEMI na Wakuu wa
Mikoa baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi na
Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika mjini
Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhandisi Evarist Ndikilo
(Mkuu wa Mkoa wa Pwani) baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa
Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi
kilichofanyika mjini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) akisani Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa
kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo, na waliosimama ni Naibu Mawaziri na Watendaji OR TAMISEMI
wakishuhudia zoezi hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) amewaongoza wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, kupitia na kusaini Mkataba
wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi
kilichofanyika mjini Dodoma.
Akiongea na Wakuu wa
Mikoa katika ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma, Mhe. Jafo amesema maelekezo
hayo awali, yalitolewa na Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu, kuhusu
tatizo la Lishe katika Mikoa nchini ambalo nchi imekwishajitoa kulishughulikia
na kutenga fedha katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2017/2018.
“Tumesaini hii mikataba
kwa lengo kubwa la kuhakikisha kwamba Wakuu wa Mikoa kama ndio viongozi wa Wakuu
wa Mikoa, wahakikishe halmashauri zao zinaenda kutekeleza mipango yao ya bajeti
ambayo imetengwa katika halmashauri zao kwa lengo kubwa kwamba, tunaenda
kutekeleza tatizo la lishe ndani ya halmashauri zetu”
Mhe. Jafo amesema Wakuu
wa Mikoa wanayo dhamana kubwa ya kusimamia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa
vituo vya afya na suala la lishe kwa ujumla, hivyo Watendaji watoe taarifa zao
kwa Wakuu wa Wilaya kabla ya kuwasilishwa kwa Wakuu wa Mikoa kwa hatua stahiki.
“Wakurugenzi watoe
taarifa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Wilaya nao wawasilishe kwa Wakuu wa
Mikoa ili waone namna ya kuzisemea taarifa hizo”, katika suala zima la
utekelezaji wa mipango ya Serikali.
Aidha, amewataka Wakuu
wa Mikoa kuwaelekeza na kuwasimamia Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya
masuala ya lishe na ujenzi wa vituo vya afya kwani mpaka sasa jumla ya vituo
2011 vimepanuliwa na kujengwa ili kutoa huduma bora kwa jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
Dkt. Kebwe S. Kebwe amesema, anaipongeza Serikali kwa kutoa takribani shilingi
11.6 Bilioni kwa ajili ya suala la lishe hasa katika kipengele cha udumavu.
Aidha, amesema suala zima
la upatikanaji wa chakula mkoani Morogoro sio tatizo bali ni elimu ya ulaji
chakula ndiyo inapaswa kutolewa ili kupunguza utapiamlo lakini pia kumekuwepo
na tatizo la Maafisa Lishe katika halmashauri nchini kupangiwa kazi nyingine,
kwa mfano kufanya kazi ya Idara tofauti kama vile kukusanya kodi.
Naye Stephen Motambi,
Kaimu Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI,
amesema suala la Lishe limekuwa likifanyika katika Mikoa na Halmashauri zote
katika kukabiliana na tatizo hili lakini kwa hivi sasa hali ya udumavu ni
asilimia 34 hivyo mikoa inapaswa kuweka mikakati kuhusiana na kuondoa kabisa
tatizo la lishe.
No comments:
Post a Comment