Mwakilishi
wa Mkurugezi wa Misitu na Nyuki, Deusdedit Bwoyo
Mkurugezi
kutoka TAMISEMI, Eng. Enock E. Nyanda
Mtendaji
Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo
Wakuu
wa wilaya,
Katibu
Mtendaji wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dr. Tuli Msuya
Mameneja
na Maafisa Misitu,
Wanahabari
Wageni
waalikwa,
Mabibi
na Mabwana.
Ndugu Washiriki,
Awali
ya yote Napenda kushukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika salama katika
kikao hiki muhimu. Aidha, napenda kuwakaribisha katika Mkoa wa Dodoma na
kuwatakia makazi mema wakati wote mkiwa hapa. Daima ni faraja na furaha kwetu
kuwa nanyi katika mkutano huu. Isitoshe kwasasa tunao uzoefu wa kupokea wageni
wa aina mbalimbali na kutoka sehemu mbalimbali. Aidha tunayo miundo mbinu ya
kutosha kuwawezesha kuishi hapa kwa amani na kufanya kazi zenu kwa ufanisi
mkubwa.
Ndugu washiriki,
Napenda
kuchukua fursa hii kuwashukuru Wakala wa Haduma za Misitu Tanzania kwa kuandaa
Mkutano huu, ambao ndio nguzo muhimu ya utekelezaji wa Randama ya makubaliano.
Kushiriki kwenu kwa wingi katika Mkutano huu ni ishara njema ya kutimiza azma
ya hutatua changamoto zinazokabili sekta ya Misitu Tanzania.
Ndugu washiriki,
Nimeambiwa
washiriki watakuwa ni Mameneja wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania, Maafisa Misitu wa Wilaya na Washauri wa Maliasili wa
Mikoa inayounda Kanda ya Kati (Dodoma, Manyara na Singida). Aidha washiriki
wengine ni Wakurugezi kutoka Ofisi ya
Rais TAMISEMI na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu kutoka Makao Makuu.
Nimeelezwa pia kwamba madhumuni ya mkutano huu
ni utekelezaji wa Randama ya makubaliano iliyosainiwa kati ya Wizara ya
Maliasili na Utalii na Ofisi ya Raisi TAMISEMI ili kuimarisha usimamizi wa Misitu
nchini na utawala bora, kufanya uperembaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko wa
misitu Tanzania na kuboresha ukusanyaji,
ugawaji, utumiaji na ufuatiliaji wa matumizi ya asilimia tano ya tozo ya
upandaji miti.
Ndugu Washiriki,
Katika
mkutano huu mtapata nafasi ya kushiriki, kusikiliza na kujadiliana kwa kina
mada zifuatazo:- Hali ya usiamizi wa misitu Tanzania; utekelezaji wa Maazimio
ya kikao cha kwanza cha Ushirikiano; Taratibu za uvunaji na usafirishaji wa
mazao ya misitu kutoka misitu ya Asili; Randama ya makubaliano na Ufafanuzi wa
sheria; Utekelezaji wa Makubaliano ya kuboresha ukusanyaji, ugawaji matumizi na
Ufuatiliaji wa 5% fedha za tozo ya upandaji miti.
Ndugu washiriki;
Kama
mnavyofahamu Misitu ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa mbili;-
i.
Uharibifu mkubwa wa misitu unaofikia kiasi
cha hekta 372,000 kwa mwaka,
ii.
Mahitaji ya mazao ya misitu kwa mwaka kuzidi
uwezo wa misitu kwa zaidi ya meta za ujazo milioni 19.5.
Changamoto
za usimamizi wa misitu zilizopo Kanda ya kati ni Pamoja na:
1 Uvunaji
holela wa mazao ya misitu na biashara ya mazao hayo isiyofuata Sheria na
taratibu.
2 Utegemezi
mkubwa wa misitu kwa ajili ya nishati (mkaa na kuni)
3 Ukataji
ovyo wa miti unaotokana na kilimo cha kuhamahama hususan kwa ajili ya kilimo,
makazi na biashara.
4 Uchomaji
holela wa moto katika maeneo ya misitu
5 Kuongezeka
kwa mahitaji ya mazao ya misitu yanayotokana na kuongezeka kwa watu na kiwango
kidogo cha upandaji wa miti.
6 Rasilimali
za misitu kuwa katika Usimamizi wa wadau mbalimbali bila uratibu imara.
7 Uvamizi
wa misitu ya hifadhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji wa mifugo.
8 Uchache wa vitendea kazi (magari na pikipiki).
9 Uchache
wa Rasilimali watu (na baadhi ya watumishi sio waaminifu).
Ndugu washiriki,
Faida
za Misitu kitaifa na kimataifa zinajulikana ikiwa ni [pamoja na kuhifadhi
udongo, upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali, ufugaji wa nyuki hivyo
upatikanaji wa asali, nishati, upatikanaji wa mvua, na kukabiliana na
mabadiliko ya tabia ya nchi. Hivyo juhudi za pamoja zinatakiwa katika kulinda
na kuhifadhi misitu yetu. Kwa kulitambua hili, ndio maana Wizara mbili;
Maliasili na Utalii na Ofisi ya Raisi – TAMISEMI
zilisaini Randama ya makubaliano ili kuunganisha nguvu pamoja katika kuzikabili
changamoto zinazokabili sekta ya Misitu hapa nchini.
Ndugu washiriki,
Napenda
kuchukua fursa hii pia kuwaasa watumishi wa misitu chini ya TFS na wa Tamisemi
ambao ndio watekelezaji wakuu wa Randama katika ngazi za Wilaya kutekeleza
kikamilifu maelekezo yote yaliyopo katika Randama ya Makubaliano iliyosainiwa
na Wizara hizi mbili ili kufikia malengo tarajiwa kwa ufanisi zaidi.
Ndugu washiriki,
Katika
mkutano huu pamoja na mambo mengine mtajadili masuala mbalimbali kuhusu
Usimamizi wa misitu na majukumu ya kila mdau katika kuhifadhi na kulinda misitu
iliyopo Kanda ya Kati. Nimatumaini yangu na ninawasihi kwamba mikakati na
maazimio mtakayojiwekea haitabaki katika mashelfu/makabati katika ofisi zenu
bali itakuwa kwenye utekelezaji wa kazi zenu za kila siku. Aidha, nashauri
mikakati mtayopanga ilenge kuwashirikisha wananchi katika Usimamizi wa
Rasilimali za Misitu hapa nchini kwa malengo na matumizi endelevu.
Ndugu washiriki,
Kwa
kuzingatia umuhimu wa hifadhi za misitu nchini, ni vyema kila mwananchi akazingatia
maagizo ya Serikali pamoja na kufuata sheria za nchi zinazohusiana na uhifadhi
na Usimamizi wa Maliasili zetu. Ningependa kuwaasa na kuagiza kuwa ni marufuku
mtu yeyote kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi za misitu na kama
kuna watu wanaendesha shughuli hizo naagiza waondoke mara moja, kabla Sheria
haijachukua mkondo wake.
Ndugu washiriki,
Baada
ya kusema haya ninatamka rasmi kuwa “Mkutano wa utekelezaji wa Randama ya makubaliano kuimarisha Usimamizi
wa misitu nchini na utawala bora baina ya Wizara ya Malisili na Utalii na Ofisi
ya Raisi TAMISEMI” umefunguliwa rasmi.
ASANTE SANA KWA KUNISIKILIZA
No comments:
Post a Comment