Hayo yamebainiswa leo katika ukumbi wa Mikutano ulioko kibamba CCM ambapo ndio makao makuu ya Manispaa hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi *John Lipesi Kayombo*.
Wakiwa katika ukumbi huo wataalamu kutoka Benki ya Dunia wakiongozwa na *Mr Moht Generiwala Director Urban Infrastructure advisory* wamefanya mazungumzo na kubadilishana " Concept note" ya maeneo ambayo Ubungo imejipanga kuwekeza.
Wakiwa katika mazungumzo hayo timu ya uwekezaji katika Manispaa ya Ubungo ikiongozwa na Mchumi wa Manispaa Ndg *Erick K. Kilangwa* walielezea kwa kina maeneo ambayo kwa sasa yanaweza kuwekezwa na baadae timu ya wataamu kutoka Benki ya Dunia na wataalamu wa Manispaa wakafanya ziara ya kutembelea maeneo hayo.
Maeneo hayo ni:
*Kituo cha Daladala SIM 2000* eneo ambalo uwekezaji wa jengo kubwa "mult complex" na Soko la kisasa unaweza kufanyika.
*Ofisi ya Kata Ubungo* katika eneo hilo uwekezaji unaoweza kufanyika ni kujenga jengo kwa ajili ya ofisi mbalimbali " re development of officies".
*Soko la Shekilango* Hapo uwekezaji wa Soko la kisasa ambalo litakuwa na tija kwa Manispaa na Wananchi kwa ujumla.
*Mburahati* (construction of Stadium )katika eneo hilo kuna kiwanja cha mpira ambacho kikiendelezwa kitakuwa na tija kwa wananchi wa Manispaa ya Ubungo.
Hayo ndio maeneo ambayo wataamu hao wamejadiliana kuona namna ya kufanya uwekezaji kwa maendeleo ya Manispaa na wananchi wake.
*Manispaa ya Ubungo imejidhatiti kuendelea kuibua fursa zilizoko na inawakaribisha watu wote wenye nia ya kuwekeza Ubungo Karibuni sana*
Imetolewa na:
*Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo*
No comments:
Post a Comment