Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Maendeleo ya sanaa Bibi. Leah Kihimbi akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akihamasisha wadau kuchangia ili kufanikisha usiku wa kitendawili utakaohimiza uzalendo kwa watanzania leo wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku huo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaonyesha wajumbe (hawapo pichani) kitabu kilichoandaliwa kuhimiza kampeni ya uzalendo na utaifa wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea tuzo ya kimataifa waliyotunukiwa PSPF kama taasisi mahiri barani Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu PSPF Bw. Adam Maingu (kushoto) wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wapili kulia ni Mtendaji Mkuu PSPF Bw. Adam Maingu
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………………………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 25/11/2017
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi zake imetangaza kampeni ya kitaifa ya uzalendo ambayo wizara kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni imeamua kuzindua kampeni hiyo kwa ajili ya kuhimiza uzalendo na utaifa katika taifa letu.
Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi cha uzinduzi wa kampeni ya uzalendo leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wizara inaona ni muda muafaka sasa kuonyesha njia sahihi ya kujenga nchi kwa kuhimarisha uzalendo na utaifa.
“Mhe. Rais amesikika mara nyingi sana akitoa wito kwa watanzania kuimarisha uzalendo na utaifa, tunahitaji kutoa elimu kwa vijana ili wajue tulikotoka na tunakwenda maana vijana wengi waliozaliwa baada ya uhuru wamekua wakiuliza mara nyingi uzalendo ni nini, na vijana hawa ndio ambao tunatarajia waongoze nchi katika karne hii” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa watanzania kama taifa moja wanawajibu wa kurithisha kizazi cha sasa yale wanayoyajua ya nyuma ili kulihimarisha taifa kuwa moja, na lenye msimamo mmoja na ambalo litaleta faida kwa watanzania wote kwa misingi iliyojengwa na waasisi wetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa watanzania hawana budi kuthamini nchi yetu kwa kuendeleza kauli mbiu ya kampeni ya kitaifa ya uzalendo inayosema nchi yangu kwanza.
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Kila mtanzania anapaswa kujiona yeye ni wakwanza katika kuhakikisha
dhana sahihi ya uzalendo inawafikia watanzania wote na kujiweka katika nafasi ya kutambua yakuwa anakwenda kuokoa kizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wazalendo, wanakua katika maadili na wanaepukana na mmomonyoko wa maadili unaoletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kampeni ya uzalendo itatanguliwa na vipindi mbalimbali kwenye redio na televisheni, makala mbalimbali, kuelezea tulikotoka, kuhamasisha utamaduni wa mtanzania, kuonyesha taifa limeegemea katika misingi ipi na kuonyesha umuhimu na ulazima wetu katika kufuata misingi hiyo.
No comments:
Post a Comment