Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka MNEC ambae katika hotuba yake aligusia mambo yafuatayo:
" Miaka miwili ya utawala wa Rais Dk John Pombe Magufuli ni kielelezo na kipimo kwa kiongozi mzalendo , mtumishi mwenye malengo na aliyekubali kujitolea muhanga kupigiania maslahi ya umma bila kutikisika" Shaka
"Utendaji huo wa Serikali tokea aingie madarakani kidomekrasia miaka miwili iliopita licha ya kuliitikisa Bara la Afrika, wameviteka vyombo vya habari duniani kwa majadiliano ya kina na uchambuzi" Shaka
"Ujasiri na uthubutu aliouonyesha Rais wa kuwashughulikia wafanyakazi hewa, watumishi wenye vyeti bandia, kuwatumbua watendaji wazembe na wengine kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu na uhujumu uchumi , umefungua ukurasa mpya wa ajabu" Shaka
"Haikuwa rahisi ndani ya miaka miwili Serikali ifufue shirika la ndege, kununua ndege mpya, kuanzisha ujenzi wa reli ya kutumia umeme, kuongeza ukusanyaji mapato ya kodi na kushughulilikia mikataba mibovu ya madini" Shaka
"Dk Magufuli anastahili pongezi kwa kuonyesha uongozi wa kizalendo kwa Taifa lake, nafikiri amewaamsha hata waafrika wenzake." Shaka
"Ameithibitishia dunia akitaka rasilimali za Afrika ziwanufaishe wananchi masikini na wayonge " Shaka .
" Vijana tunaridhishwa na mikakati ya kuwadhibiti mchwa wala ruzuku za serikali kwenye halmshauri za wilaya na kufuja miradi ya maendeleo huku Rais akihimiza nchi kuwa ya viwanda kuelekea uchumi wa kati" Shaka
"Amerudisha nidhamu ya kazi na kukuza utendaji wenye ufanisi sambamba na kukomesha uvivu, uzembe na utoro maeneo ya kazi " Shaka
"Vijana wa Tanga muungeni mkono rais wa kuwa wazalendo, kufanya kazi kwa bidii kujituma na kutumia vyema fursa za kiuchumi mkoani kwenu hapa na maeneo ya jirani" Shaka
" Ujio wa bomba la mafuta, uanzishwaji wa kiwanda kikubwa cha saruji afrika mashariki ni hatua nyengine ya kusongeza na kupunguza kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana" Shaka
"Mumebahatika kuwa na Mkuu wa mkoa mzuri sana Martin Shigela unaumwa na vijana sababu ameandaliwa vyema na UVCCM na sasa amewiva mpeni ushirikiano mtapiga hatua kubwa za kimaendeo Vijana" Shaka
" Rais Magufuli ameinua kiwango cha uwajibikaji, serikali yake inajiendesha kwa uwazi , uaminifu na uadilifu miiko na maadili ya uongozi sasa inaheshimiwa " Shaka
"Ikitokea Baba wa Taifa kama atafufuka hatataka kuondoka tena kwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yaliyofikiwa katika Taifa letu" Shaka
" Ndani ya kipindi cha miaka miwili iliopita serikali imedumisha mahusiano mema na nchi jirani" Shaka
"Nchi wahisani na washirika wa maendeleo sasa wanamfata Rais nchini na tulizowea viongozi wetu kuwafata wao jambo ambalo limeendeleza kufungua mahusiano na milango ya kiuchumi " Shaka
"Tumepata serikali inayowajibika kwa wananchi imepunguza maonevu, manyanyaso na sasa kila mmoja ana haki mbele ya sheria na katiba ya nchi" Shaka
"Serikali imewathibitishia maadui wa muungano walioko ndani na nje wakithuhutu kuutikisa watashughulikiwa" Shaka
"Mwenyekiti wa ccm Rais Magufuli ameendeleza msisitizo wake huku akiwataka wananchi na viongozi wa kisiasa kuweka kando itikadi za vyama badala yake wajali uzalendo na maendeleo kubadili sura ya nchi toka kwenye kadhia ya umasikini na kupata neema." Shaka
"Vijana tutazidi kukimbizana na kasi ya Rais wetu ili kufanikisha malengo yetu kisiasa, kijamii na kiuchumi. Unapokwisha uchaguzi mwelekeo wa pamoja ni mkazo katika maendeleo na si porojo tena za kisiasa na mikutano ya hadhara yenye matusi na idhara " Shaka
No comments:
Post a Comment