Mkurugenzi
mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi Mkuu wa Shule
ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote baadhi ya vitabu
kwaajili ya wanafunzi kujisomea na kuongeza maarifa kupitia vitabu hivyo
ambavyo vimetolewa kwa msaada na benki ya UBA Tanzania
Mkurugenzi
Mkuu wa benki ya UBA Tanzania akiongea na mkuu wa shule ya sekondari ya
Barbro Johanson pamoja na wafanyakazi wa benki ya UBA na shule hio mara
baada ya kukaribishwa ofisini kwa mkuu wa shule hiyo Bi Halima Kamote
mapema jana
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiangalia
moja ya vitabu mia nane vilivyotolewa na benki ya Uba katika kuendeleza
juhudi zao za kurudisha faida kwa jamii. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya UBA Tanzania Bw Peter Makau.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiongea na
wafanyakazi wa benki pamoja na shule hio katika ofisi yake mara baada ya
kupokea ugeni kutoka benki ya UBA Tanzania ambao walifika shule hapo
kwaajili ya kukabidhi msaada wa vitabu takribani mia nane vya kujisomea
msaada ambao umekabidhiwa kwa mkuu wa shule hio.
Imeandikwa na Josephat Lukaza
Katika
kuendeleza kwake kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kusoma na kupata
vifaa mbalimbali vya kukuza taaluma zao, Mapema jana benki ya Uba
Tanzania walitoa msaada wa Vitabu takribani 800 za kiada ambazo
vitasaidia kuongeza hali ya usomaji kwa wanafunzi wa shule hio.
Msaada
huo wa vitabu zaidi ya mia nane ulitolewa mapema jana shule hapo na
kukabidhiwa mkuu wa shule hiyo Bi, Halima Kamote huku Mkuu wa shule hio
akiishukuru benki hio kwa kujitoa kwake katika kusaidia kuongeza vitabu
vya kujisomea kwa wanafunzi wa shule huku akisema amefurahishwa na benki
hio kwa msaada huo na kuwakaribisha tena pale ambapo wataguswa
kuchangia zaidi na zaidi.
Naye
mmoja wa wanafunzi aliyepokea kitabu kwa niaba ya wanafunzi wenzake
ameishukuru pia benki ya UBA kwa msaada huo wa vitabu kwa maana
itaongeza hali ya kujisomea na kuongeza ujuzi katika mawasiliano ambapo
somo la Ujuzi wa Mawasiliano limekuwa moja ya somo katika Shule hiyo
huku likiwa halipo kwenye mitaala ya kufundishwa katika shule za
sekondari hapa Nchini.
Benki
ya Uba imekuwa moja ya benki ya kibiashara hapa nchini katika Kuchangia
maswala mbalimbali ya kijamii huku ikirudisha faida yake kwa jamii
iliyowazunguka.
Mkurugenzi
mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi mmoja wa
wanafunzi wa shule ya Barbro Johanson moja ya vitabu vilivyotolewa na
benki hio kama mchango wake kwa jamii. Picha na Josephat Lukaza – Lukaza
Blog
No comments:
Post a Comment