Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga ukuta katika kituo cha afya Mganza Halmashauri ya Wilaya Chato. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mganza (Chato) alipofanya ziara ya kikazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo. |
Akina mama wa kijiji cha Ilyamchele Wilayani Chato wakishiriki katika ujenzi wa vyumba viwili na Ofisi shule ya Msingi Ilyamchele kwa kusogeza matofali kwa mafundi wa ujenzi.
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya
madarasa na Zahanati Wilayani humo.
Mhandisi Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na
wananchi kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili
pamoja na Ofisi katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la
wanafunzi 2,212 kutoka 1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao wanasoma
kwa awamu mbili hivyo, kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya vyumba vya
madarasa 28.
Akizungumza na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema
kuwa Serikali inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine
kwa kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na
walimu wa kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na
viongozi wote katika utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa vyumba vya
madarasa na Zahanati.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo
ameshiriki katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya wananchi
kupata huduma katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na vituo vipya vya
afya.
Miradi hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa
kujitolea kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula
wanapokuwa katika eneo la kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta maji,
mchanga, sementi, kokoto na kushiriki katika ujenzi.
Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa
Mkoa baada ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina
kuhusu mikakati na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na
Zahanati kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa
Tarafa, Maafisa elimu wa Wilaya na Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.
No comments:
Post a Comment