Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua baadhi ya vitendeakazi mara baada ya kutembelea Maabara ya Uchambuzi wa Viuatilifu katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki (TPRI) kilichopo Mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua baadhi ya mbegu za maharage zilizogunduliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na watumishi katika Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) wakati wa kikao cha kazi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mansoor akielezea jambo mbele ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) Dkt Margaret J. Mollel kukagua maabara ya uchambuzi wa Viuatilifu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua
baadhi ya mbegu za maharage zilizogunduliwa na Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mansoor akielezea jambo wakati wa kikao cha kazi na Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo Selian Kanda ya Kaskazini (NZARDI) mara baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Ukaguzi wa vifaa kazi katika sekta ya kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akipata maelezo ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Maabara ya Uchambuzi wa
Viuatilifu katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti
visumbufu katika ukanda wa Tropiki (TPRI) kilichopo Mkoani Arusha.
Na Mathias Canal, Arusha
Taasisi za utafiti katika sekta ya
kilimo zimetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha
wakulima kote nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika
ipasavyo.
Wataalamu wa utafiti wamepaswa
kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti ikiwemo Kuongeza ujuzi
katika Utafiti wa mazao mbalimbali wasiishie katika zao moja au mawili tu.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe alipotembelea Taasisi ya Utafiti ya
viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki iliyoanzishwa mwaka
1945 yenye jukumu la kuendeleza utafiti na kutoa huduma za matumizi sahihi na
salama ya viuatilifu, Taasisi ya utafiti na Mafunzo ya Tengeru, HORTI Tengeru
iliyoanzishwa mwaka 1980 sambamba na Kituo cha Utafiti wa kilimo na Maendeleo
Selian (SARI) kilichofunguliwa mwaka 1979 kama shamba la utafiti wa ngano na
Shayiri chini ya ufadhili wa Canada.
Mhandisi Mtugumwe aliwasihi watafiti
hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali kwa ajili ya
kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani bajeti ya serikali pekee
haiwezi kutosha.
Alisema wataalamu hao wanapaswa kufanya
tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli.
Alisema Wizara ya kilimo ipo tayari
kuwakaribisha baadhi ya watafiti kwenye kamati ya Bunge inayoshughulikia kilimo
ili kuwasilisha vitu walivyovifanya katika Utafiti mbele ya wabunge ambaomoja
ya jukumu lao kubwa ni kutunga sheria.
Kuhusu changamoto za nyumba za
wafanyakazi alisema kuwa tayari zipo katika Taasisi na vyuo vyote vya Utafiti
hivyo itakapofanywa tathmini yote kwa ajili ya vyuo vya kilimo nchini litatekelezwa
pia katika chuo hicho.
Mhandisi Mtigumwe alisema watafiti
hao wanapaswaKuwa na mikakati ya kupata vijana wengi zaidi ili waweze kujifunza
fani hiyo kuhusu Utafiti kwani bado serikali inatambua kuwa vijana ndio
nguvu kazi ya Taifa.
Kuhusu mpango wa Wizara ya Kilimo
kwenye Mazao ya mboga mboga na matunda alisema kuwa ni sehemu ya kipaumbele cha
Wizara na serikali.
Katika hatua nyingine alisema
atawasaidia kutengeneza kitalu nyumba (Green House) kimoja kwa ajili ya kujifunzia
MWISHO.
No comments:
Post a Comment