Saturday, November 4, 2017

MFUKO WA JIMBO ILEMELA KUPUNGUZA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Jimbo la Ilemela limepokea kiasi cha fedha chenye jumla ya shilingi Milioni 29 kupitia mfuko wa Jimbo

Akizungumza katika kikao cha mfuko wa Jimbo Jimbo la Ilemela Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa Jimbo lake limepokea kiasi cha shilingi  Milioni 29 Laki 8na Elfu 63 kama fedha za mfuko wa Jimbo ambapo kupitia kikao cha mfuko wa Jimbo kimeamua fedha hizo zitumike kwaajili ya kufyatulia matofali yatakayotumika kutengeneza Vyumba vya Madarasa ili kupunguza adha ya Upungufu wa madarasa

'... Tumepokea zaidi ya Milioni 29 kama fedha za mfuko wa Jimbo na kupitia kikao cha mfuko wa Jimbo tumependekeza fedha hizo zikasaidie kupunguza changamoto mbalimbali kwa kadri tutakavyokuwa tunazipokea lakini tukianza na hili la upungufu wa madarasa kwaajili ya wanafunzi wetu kwa kata zote ...' Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula ameongeza kuwa kikao cha mfuko wa Jimbo kimezitaka kata zote za Jimbo la Ilemela kupitia madiwani wake na watendaji kuhakikisha wanaitumia vizuri fursa hiyo huku akisisitiza kuwa ugawaji wa fedha hizo utategemea utayari na kasi ya mitaa au kata katika kutimiza masharti ya kipaumbele cha kupewa tofali hizo ambacho ni kuanza msingi na kukaguliwa kupitia kibali cha mhandisi wa manispaa ya Ilemela

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
04.11.2017

No comments:

Post a Comment