Askari wa jeshi la Syria (Hapa ilikua Deir Ezzor Oktoba 31, 2017).
Majeshi ya Syria yakisaidiwa na kundi la Hezbollah kutoka Lebanon na
wanamgambo wa Iraq wameurejesha tangu siku ya Jumatano jioni mji wa
Al-Bukamal kwenye himaya ya serikali kutoka mikononi mwa kundi la
Islamic State.
Al-Bukamal ni mji wa mwisho ambao ulikua
ukishikiliwa na kundi la Islamic State mashariki mwa Syria. Taarifa ya
kuurejesha mji huu kwenye himaya ya serikali imethibitishwa na vyanzo
vya serikali vya Syria na shirika la la habari la Urusi la Sputnik.
Jeshi la Syria lilitarajia vita vikali
na vya muda mrefu kwa minajili ya kuurejesha kwenye himaya yake mji wa
Al-Bukamal, ambapo walikua walijificha wapiganaji wa mwisho wa kundi la
Islamic State, ambao walikimbia mkoa wa Syria wa Deir Ezzor na mji wa
Iraq wa Al-Qaim. Lakini wapiganaji hao wamepoteza mji huo kwa haraka
kuliko ilivyotarajiwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi kutoka
Syria, Urusi na Syria walitumia uwezo mkubwa katika vita vya kuurejesha
mji huo kwenye himaya ya serikali. Kikosi cha wanamaji na kile cha
wanaanga walirusha makombora mengi na mabomu wiki mbili zilizopita dhidi
ya ngome za kundi la Islamic Islamic.
Pamoja na kupoteza mji wa Al-Bukamal,
kundi la Islamic State halina tena mji wowote linaloshikilia nchini Iraq
na Syria. Lakini wapiganaji wa kundi hilo wapo katika maeneo makubwa ya
jangwani kati ya nchi hizo mbili, ambako wamehifadhi chakula, silaha,
na risasi, kwa kutarajia vita ya vya kuvizia katika nchi hizo.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment