Wednesday, November 22, 2017

KAFULILA NAYE ATIMKA CHADEMA, KUTANGAZA CHAMA ANACHOENDA HIVI KARIBUNI

Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila amejivua uanachama wa Chadema kwa madai upinzani hauwezi kuendesha vita dhidi ya ufisadi.

Hatua hii inajiri baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kusema kwamba kisasi cha CCM kuchukua wanachama wake kitasaidia kuwaondoa wavulana kwenye mapambano ya siasa za upinzani.
Lema ameyasema hayo ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Patrobas Katambi kuomba kuomba ridhaa ya kuingia ndani ya Chama cha Mapinduzi leo katika kikao cha halmashauri Taifa.

Lema amesema kwamba CCM imekuwa na kisasi kikubwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili mstaafu na Mbunge wa Singida Kaskazini  Lazaro Nyalandu kuondoka CCM 

"Baada ya Lazaro kuondoka CCM , CCM wamekuwa na kisasi kikubwa , ambacho kimsingi kitasaidia kuondoa wavulana ktk mapambano haya , bado Mameya wawili ? Na kijana mwingine aliyekuwa shupavu 2010-2015. Msiogope kwani wanawaogopa sana na ndio sababu ya matendo haya" Lema.

No comments:

Post a Comment