Sunday, November 5, 2017

HATIMAYE MWANAUME ALIYEZALIWA BILA MAPAJA APATA MCHUMBA



Mrembo Chelsee Stuart (19) akiwa na mumewe Nathan Hrdlicka (34) wakiwa kwenye pozi la mahaba.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Nathan Hrdlicka (34) alimpata mpenzi wake huyo aitwae Chelsee Stuart (19) kupitia mtandao wa facebook na baadae kukutana nae mjini Santa Fe nchini Mexico na kumvisha pete ya uchumba rasmi.

Nathan mwenye urefu wa futi 4.6 alikuwa akitaniwa na watu mtaani kwake kuwa ni mbilikimo na kujikuta akikataliwa na kila mwanamke aliyejaribu kumchumbia.

Hata hivyo, mwanamke huyo mwanzoni alimchukulia Nathan kama mlemavu lakini kadri siku zilivyozidi kwenda alijikuta akifurahia mahusiano yao.

Tatizo alilozaliwa nalo Nathan kitaalamu linaitwa Tbilateral Proximal Femoral Focal Deficiency (TPFD) ambapo watu 25 tu duniani ndio wamezaliwa na tatizo hilo.

Kati ya watu hao 25 ni yeye pekee ndiye aliyefanikiwa kutembea ingawaje anapata changamoto kubwa ya kusuguana kwa mifupa kwenye eneo la kiuno.

“Nasikia kuna watu 25 tu hapa duniani wenye hali kama yangu lakini ni mimi pekee mwenye uwezo wa kutembea hilo jambo linanifanya nijione mwenye bahati. Ingawaje sio kwa umbali mrefu wala sio kila siku lakini kwani nikifanya hivyo huwa napata maumivu makali kiunoni kwani kuna msuguano kati ya mifupa ya miguu na kiuno.”amesema Nathan kwenye mahojiano yake na Daily Mail.

“Sijioni kama nina utofauti mkubwa na wenzangu, ingawaje kila ninayekutana naye kitu cha kwanza anaangalia ulemavu wangu na mimi sijali hilo. Kwa sababu ulemavu haunielezei mimi jinsi nilivyo moyoni“amesema Nathan.

Tazama picha za wawili hao jinsi walivyopendeza.

No comments:

Post a Comment