MANUFAA
ya uchumi unaokua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda
hayataonekana kama taifa litakuwa na changamoto katika utengenezaji wa
miji yake na hivyo kuvuna tija ya miji iliyopangwa vyema.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya
Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy wakati akifungua mkutano wa
wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania
(Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF).
Mkutano
huo ulikuwa na lengo la kuangalia mada tatu zilizokubaliwa kufanywa
kama sehemu ya kutengeneza mwongozo wa namna ya kuendesha mpango huo ili
kuisaidia serikali katika kutengeneza miji salama na yenye tija.
Mada
hizo tatu ni pamoja na kuangalia miundombinu ya miji na huduma za
kifedha katika utengenezaji wa miji, mahusiano ya serikali kuu na ya
mitaa ; na mada ya tatu ni namna ya kupata taarifa sahihi ili kuimarisha
uwekezaji.
Kessy
alisema wakati serikali inatekeleza malengo ya mpango wa pili wa
maendeleo wa miaka mitano (FYDP) ll , wenye lengo la kuweka mazingira
sawa kwa uchumi wa viwanda na maendeleo, mpango huo wa ESRF umekuja muda
muafaka kwani utasaidia kutafuta na kutoa majawabu halisi na sahihi.
Alisema
kwamba kama nchi itataka kuwa na maendeleo yenye kujali binadamu ni
vyema kuwa na maamuzi ya miongo yenye kuakisi uhalisia na mahali pekee
kwa sasa kupata huo uhalisia ni wa kutumia mpango huo wa ESRF ambapo
wanazuoni watakutana kujadili uhalisia wa mambo na kutoa mapendekezo ya
kukabili changamoto.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida alisema mkutano huo ambao ni
wa kwanza tangu alipoamua kuwa na Tanzania Urbanisation Laboratory,
Agosti mwaka huu umelenga kusaidia kutengeneza njia ya kusaidia
utengenezaji wa miji salama yenye tija nchini.
Alisema
kwa kuwa mwenyekiti wa mpango huo ni Tume ya Mipango wao wakiratibu tu,
ni dhahiri mawazo na mapendekezo yatakayokuwa yanatolewa kulingaana na
utafiti yatasaidia sana kuwa na miji salama.
No comments:
Post a Comment