Jumuiya ya watanzania
wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora
Caucus Washington kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kutatua changamoto za ofisi za
walimu wa mkoa huu kwa kutoa makontena 36 ya samani mbalimbali
zikiwemo viti vya kisasa zaidi ya 5000, meza za umeme 2500,meza za
kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za
kuandikia 700.
Mchango huu wa samani
ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani $ 800,00 ambazo ni
sawa na shilingi 1,800,000,000 za kitanzania utatumika katika ofisi
mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na Mh Paul Makonda mapema Agosti mwaka huu.
Kupitia samani hizi
adhma ya Mh Paul Makonda ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji
wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa
kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha ufaulu wa
wanafunzi kufikiwa kama matokeo ya miundo mbinu rafiki kwa wote.
Makontena hayo yanatarajiwa kufika nchini mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mh Makonda amewashukuru wadau hawa ambao bila kuzingatia umbali waliopo na nchi yao
bado wameonyesha hari ya kuguswa na changamoto za watanzania wenzao
hapa nchini, na kutoa rai kwa watanzania wengine kuendelea kuunga mkono
kampeni hii ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam kwa namna
watakavyo weza kwani hatma ya ustawi wa maendeleo ya Tanzania ni wajibu
wa kila mtanzania.
No comments:
Post a Comment