Saturday, November 11, 2017

DC NGUPULA, COSTEC NA CHUO CHA UTAFITI MARUKU WAFANIKIWA KUTOA MBEGU ZA MIHOGO

Na Mwandishi Wetu, Tabora

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula kwa kushirikiana na COSTEC na Kituo cha Utafiti cha Maruku kilichopo mkoani Kagera  wamefanikiwa kutoa Mbegu za Mihogo zenye uwezo wa kuzalisha hadi Tani 60 kwa hekari moja pamoja na mbegu za viazi lishe (muhimu sana kwa lishe haswa kwa watoto wa umri wa kwenda shule).

Mbegu hizo zitagawiwa kwa vijiji vitano wilayani humo ambavyo vitakuwa shamba darasa kwa kujionea ubora wa mbegu hizo lkn pia kama chanzo cha mbegu kwa watu wengne baada ya kuhamasika.

Wilaya ya Nzega ni moja za wilaya zinazoathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupata mvua chache sana (wastani wa 660mm) tofauti na miaka ya nyuma ambapo wilaya hii ilipata mvua zaidi ya 1600 mm. Sifa kuu ya mbegu hizo ni uwezo wake wa kustahimili ukame kiasi lkn pia ni nzuri kwa uzalishaji mwingi kwa hekari.

Juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Nzega zinalenga katika kuhakikisha kunakuwepo na chakula cha kutosha katika kila kaya wilayani hapa na hivyo kuhimiza sana angalau kila kaya iwe na nusu hekari ya mihogo na nusu hekari ya viazi lishe.

Katika kusisitiza hilo alisema: Nataka tuwe na chakula cha kutosha wilayani kwetu na msimu ujao wilayani kwangu ni lazima shule zote watoto wale chakula shuleni. Hivyo basi ni muhimu kila mtu awe na shamba kwa ajili ya chakula.

"Malengo yetu ni kuhakikisha tunakua na Chakula cha kutosha; na tumeamua kuhakikisha hili linafanikiwa kupitia utoaji wa mbegu hizi na elimu nzuri ya upandaji wake" alisema Ngupula.

Aidha, Mhe. Ngupula kwa kushirikiana na wakurugenzi wake wa Halmashauri ya Mji wa Nzega ( Bw. Philimon Magesa)  na wa Halmashauri ya Wilaya ( Bw. Jacob Mtalitinya) wameamua kununua tani nyingi zaidi za mbegu hizo kwa kadri ya uhitaji wa wananchi.

Mh Godfrey Ngupula alihitimisha hotuba yake kwa kusema " Nzega yetu ni lazima tuwe na chakula cha kutosha hapo ndipo tutaona wilaya yetu ikisonga mbele kwa maendeleo"

No comments:

Post a Comment