DAR ES SALAAM
Chama
cha Labour cha nchini Uingereza kimepongeza juhudi za Rais Dk. John
Magufuli na Serikali yake ya awamu ya tano kwa utendaji mzuri katika
kulinda na kugawanya rasilimali za nchi kwa watu wake.
Pongezi
hizo zimetolewa hivi karibuni na Viongozi wa Labour Party katika
Mkutano na vyama mbali mbali vya kisiasa vikiwemo vya Kiafrika vya CCM,
SWAPO na ANC, uliofanyika Uingereza na kuhudhuriwa na Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Akizungumza
na mwandishi Jonas Kamaleki wa Idara ya Habari (MAELEZO) Lubinga
amesema Chama cha Labour kinataka haki sawa kwa wote, kwa hiyo kitendo
cha Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kusimamia rasilimali na
kuhakikisha rasilimali zetu zinazoibiwa zisiibiwe tena, kimewapa faraja.
Lubinga
amesema Labour Party wanaamini kuwa hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano
kujikita katika kusimamia rasilimali za nchi kitaleta maandeleo kwa kuwa
hakuna maendelo yanyoweza kupatikana bila usimamizi mzuri wa
rasilimali.
“Chama
cha Labour kinapigana kuhakikisha wananchi wake wanapata makazi bora,
hivyo suala la Accacia ambao walikuwa wakifanya vitendo visivyoendana na
hali halisi ya rasilimali hasa kwetu sisi walengwa kimewafurahisha
sana na kuona kuwa mazungumzo yamekamilika katika mazingira ya
kukubaliana namna ya rasilimali hizo zinavyotumika kuwanufaisha
Watanzania,”alisema Lubinga.
Kuhusu
mwelekeo wa uchumi, Kanali Mstaafu Lubinga amesema kuwa uchumi wa
Tanzania unakua na utakuwa wa kuvutia kwa kuwa ni juhudi za makusudi
zinafanyika hivyo amewataka wanachi wawe na subira.
Ameongeza
kuwa wazazi wawaandae watoto wao kufanyakazi na wasiwaachie tu kwenda
wanavyotaka akitoa mfano kuwa mtu akiona mtoto wake amenunua gari la
kifahari inabidi amuulize fedha ametoa wapi za kununua gari hilo wakati
mshahara wake unajulikana na ni mdogo.
Lubinga
amewataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwa mabadiliko huleta kiwewe
kwa watu na yakishaleta matokeo chanya, watu hao husahau walioleta
maendeleo hayo.
Serikali
ya Awamu ya Tano imetimiza miaka miwili tangu iingie madarakani Novemba
5, 2015. Katika kipindi hiki watanzania wameshuhudia miradi mikubwa ya
maendeleo ikianzishwa na kutekelezwa, mfano ujenzi wa barabara,madaraja,
ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa reli ya kisasa, (standard gauge),
utengenezaji wa madawati na elimu bure kwa elimu ya msingi na mwisho
nidhamu ya kazi imerejea katika utumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment