Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni
akifungua mjadala katika Siku ya Kukumbuka waathirika wa Ajali
Duniani (The World Day Of Remembrance For Road Traffic Victims 19
November 2017) iliyoandaliwa na kufanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mbio
za Magari Tanzania AAT Upanga jijini Dar es salaam ikishirikisha
wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Tanzania
Wadau mbalimbali wamekutana
na kujadiliana namna ya kupunguza ajali hasa katika kuzipitia sheria za
usalama barabarani na kuzifanyia marekebisho pamoja na kuwakumbusha
watumiaji wa Barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, Taasisi
zilizoshiriki katika mjadala huo ni WHO, KIkosi Cha Usalama Barabarani,
SUMATRA, Chama Cha Mbizo za Magari Tanzania AAT, Chama cha Kutetea
Abiria Tanzania CHAKUA, TIRA na wawakilishi Idara ya Habari Maelezo.
Mratibu wa Semina hiyo Bw.
Alferio Nchimbi akizungumza katika semina hiyo na kukaribisha wadau
mbalimbai ili kuchangia michango yao katika mada mbalimbali
zilizowasilishwa.
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akisisitiza jambo wakati akijibu maswali katika semina hiyo kulia ni Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi.
Bw. Monday Likwepa Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Abiria akichangia mada katika semina hiyo.
Bi Mary Kessi Mratibu
Programu ya Usalama Barabarani WHO akitoa mada katika semina hiyo
iliyofanyika kwenye ofisi za Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT)
Upanga jijini Dar es salaam.
Afisa Leseni Mwandamizi kutoka SUMATRA Bw. Gabriel Anthony akitoa mada katika semina hiyo.
Daktari Bingwa wa Kitengo cha
Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili Dk Juma Mfinanga akitoa
ufafanuzi kwa upande wa hospitali ya Muhimbili wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semiha hiyo
No comments:
Post a Comment