Na Tulizo Kilaga
Bwana Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mbarak Kajia ameuawa na kundi la watu wasiojulikana kwa kumpiga bwana huyo mawe na matofali sehemu mbalimbali za mwili wake alipokuwa katika harakati za kutekeleza majukumu yake, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, Prof. Dos Santos Silayo amesema tukio hilo limetokea Novemba 23 mwaka huu majira ya usiku maeneo yaKwediboma wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Taarifa hiyo inadaiwa kuwa marehemu alikuwa kwenye maandalizi ya kutekeleza majukumu yake ndipo alipovamiwa na watu hao na kuanza kumpiga ndipo marehemu kuanza kupiga yowe la kuomba msaada.
Hata hivyo taarifa ilidai kuwa watu waliamka na kufanikiwa kuwakamata watu wawili wanaoaminika kushiriki kumpiga kwa mawe na matofali sehemu mbalimbali za mwili wake kitendo kilichosababisha bwana misitu huyo kupoteza fahamu na baada ya muda mchache alifariki dunia.
Taarifa ya kaka wa marehemu aliyotoa kwenye ibada ya maziko ya Kajia yaliyofanyika kijijini kwao Romwe, Sanya, Mwanga – Kilimanjaro jana, Yusuph Kajia aliyekuwepo eneo la tukio amesema raia wema walitoa taarifa polisi ndipo askari walifika eneo la tukio na kukuta mdogo wake akiwa tayari amefariki dunia na mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Jeshi la Polisi linawashikilia watu sita kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Mtendaji Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote, akiwataka kuacha tabia ya kujichulia sheria mkononi kwani ni kosa la jinai, aidha anawataka wananchi kushiriki katika kuhifadhi maliasili za nchi kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
No comments:
Post a Comment