Waziri
wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, George Mkuchika amewaagiza waajiri wote wa serikali kuhakikisha
wanatoa vielelezo vinavyotakiwa vya watumishi wao ndani ya siku 14 pale
wanapoagizwa kufanya hivyo na Tume ya Utumishi wa Umma, kinyume cha hapo
watawajibishwa.
Mkuchika alitoa agizo hilo jana alipotembelea Tume hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa.
Aliwataka
waajiri hao kuzingatia sheria kwa kuwa imeelezwa kuwa wamekuwa ndio
chanzo cha kuchelewesha kesi za waajiriwa kwa kutokutoa ushirikiano kwa
haraka.
“Waajiri
zingatieni sheria, pale tume inapotaka kupata vielelezo inataka
ijiridhishe. Kesi zinachukua muda mrefu kama hakuna vielelezo lazima
zichelewe,” alisema Mkuchika.
Kwa
upande mwingine, aliwataka wafanyakazi wa tume hiyo kutekeleza majukumu
yao ya kazi, huku wakijiepusha na rushwa kwa kuwa eneo wanalofanyia
kazi lina ushawishi mkubwa.
Pia aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili tume hiyo zikiwemo za rasilimali fedha, watu na usafiri.
Naye
Kaimu Naibu Katibu wa Tume hiyo, Richard Odongo alisema tume hiyo
inapokea na kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma ambao
hawajaridhika na mamlaka zao za nidhamu.
No comments:
Post a Comment