Wednesday, October 18, 2017

Waziri Mkuchika afanya ziara katika Taasisi zilizo chini ya ofisi yake, Awaambia kuwa tofauti kubwa ya mishahara serikalini kukoma

1Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akieleza kuhusu utendaji wa taasisi anayoiongoza wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
2Afisa kutoka Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) akiwasilisha mada kuhusu kazi na mafanikio ya wakala wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika wakala hiyo mapema leo.
3Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifuatilia mada iliyowasilishwa kuhusu kazi na mafanikio ya TaGLA alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan P. Mlawi, na Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA, Bw. Charles Senkondo.
4Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Watumishi wa TaGLA mapema leo jijini Dar es Salaam.
5Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki (Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
6Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw. Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
7Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokewa na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
8Sehemu ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi katika ofisi za Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
9Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na watumishi wa bodi.
10Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijionea utunzaji wa kumbukumbu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Idara ya Kumbumbuku na Nyaraka za Taifa leo jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment