Watafiti,
Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia),
kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi
mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika Kijiji cha
Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha
shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo.
Mwakilishi
wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na
wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba
darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.
Mtafiti, Dk.Beatrice Lyimo kutoka COSTECH, akizungumzia kuhusu mradi huo wa mbegu bora
Mtafiti
wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani
Kagera, Josianas Kabura (mwenye mbegu), akitoa mafunzo kwa wakulima
jinsi ya kupanda mbegu hiyo ya mhogo aina ya Mkombozi iliyozalishwa
kitaalamu.
Mtafiti
wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani
Kagera, Josianas Kabura, akielekeza namna ya upandaji wa mbegu ya viazi
lishe katika kijijini cha Msenyi
Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala, akipanda mbegu hiyo katika shamba darasa kijijini Kalebezo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akipanda mbegu ya mhogo.
Ofisa Ugani, Jonas Kamugisha akipanda mbegu ya mhogo.
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kalebezo, Juster Nkuna akipanda mbegu ya mhogo.
Mbegu ya mhogo ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Kalebezo.
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Chapajembe wa Kijiji cha Msenyi, Josia Kagwingi,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe katika
kijiji hicho. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kikundi hicho, Mariana Mariko
na kulia ni mwanakikundi, Zabia Emanuel.
Mkulima wa Kijiji cha Msenyi, Martin Tibenda akipanda mbegu ya viazi lishe katika uzinduzi wa shamba darasa.
Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.
WAKULIMA
wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo
ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi
lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima
wengine katika wilaya hiyo.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno
Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba
darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
“Kwa
niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa
kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto
tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato”
alisema Ngawagala.
Ngawagala
alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia
vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji
Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo
yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi
katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya
wilaya hiyo.
Mwenyekiti
wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo
waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na
changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora
na ukame.
“Tutahakikisha
shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB
linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii” alisema
Kibuka.
Akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo
alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili
kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia
wakulima na kupata chakula cha kutosha.
Alisema
COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha
kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika
nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.
Dk.
Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani
kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na
kuzisambaza kwa wakulima wengine.
Ofisa
Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis Baraka alisema mkoa huo umepata bahati
kubwa kwa kupelekewa mbegu hizo katika wilaya tano ambapo katika kila
wilaya vijiji viwili vilichaguliwa kuanzisha shamba darasa la mbegu ya
mhogo na migomba na viazi lishe kutegemea uhitaji wa zao gani katika
kijiji husika.
“Tuna
bahati kubwa kuletewa mradi huu katika mkoa wetu hivyo tusiwaangushe
hawa wenzetu tuwe wa mfano tuyatunze haya mashamba ili tupate matokeo
mazuri” alisema Baraka.
Mtafiti
wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani
Kagera, Josianas Kabura amewataka wakulima hao kutambua kuwa mbegu hizo
za mihogo walizokabidhiwa zinatunzwa vizuri kwani zinauwezo wa kutoa
tani 32 za mhogo kwa ekari moja na kwa viazi lishe zinatoa tani 7 hadi 9
kwa ekari tofauti na mbegu za zamani ambazo hazina tija.
Mashamba darasa ya mbegu
bora za Mihogo,Viazi lishe na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa
yaliyoanzishwa katika mkoa huo yanajumuisha wilaya tano za Mkoa wa
Kagera baada ya COSTECH na OFAB kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo wa
wilaya hizo na kata zote ikiwa na lengo la kuwasaidia wakulima
kuzalisha mazao yao kwa tija na kuachana na kilimo kisicho bora na tija.
No comments:
Post a Comment