Sunday, October 22, 2017

USAHIHI NA UHALALI WA SERA NA MSIMAMO WA CCM

Mnamo mwezi wa April 2017, Kabla ya Majadiliano na Barrick walisema kwa kuzuia makinikia tutashtakiwa na kushinikiza tuachane na jambo hilo.

Ilipofika kwenye mwezi wa Julai 2017, tukaendelea kusimama imara na kuwapuuza, Mtendaji wa Barrick akaja na kukiri makosa na kukubali lazima Tanzania ipate haki yake katika uchimbaji madini. Wapinzani wakasema sio kweli na hatukuelewa kiingereza cha Bwana Thornton. Tuliwapuuza na tukaanza majadiliano kwa umakini mkubwa, kwasababu hawakujua mazungumzo yalikuwaje, wakazusha kwamba ngoma nzito, na eti majadiliano yamekwama.

Leo Mwezi wa Oktoba 2017, Majadiliano yameisha na Mtendaji wa Barrick amesema haya ni makubaliano bora zaidi kuingiwa huenda Duniani. Tanzania inapata gawio la umiliki migodi asilimia 16 na itapata gawio la faida baada ya kodi zote kukatwa la asilimia 50 na Barrick asilimia 50.

Maana yake ni 16% + 50% ya faida + Kodi zote kwa mujibu wa sheria + Bilioni 700 za awali na Mazagazaga mengine kibao kwa watanzania.

Wapinzani mufilisi wanasema eti tukatae twende Mahakamani.

Tumewashtukia, tumewang'amua mnataka kutuchezesha ngoma ya kitoto ilhali sie watu wazima.

Kwa Serikali ya CCM, Endeleeni kuchapa kazi maana 2020 tutatoa hesabu kwa ushahidi, hawa jamaa wa kuzungusha ngumi na vidole uma hawana cha kupoteza

Rais Magufuli ameshaelekeza kufumua pia maeneo mengine ya madini katika Almasi na Tanzanite ili kuhakikisha kila haki ya watanzania inapatikana. Najua katika mchakato na vita hii tutakanyaga vidole vya baadhi ya watu tunafanya kwa nia njema na maslahi mapana ya watanzania.

Waendelee kuzungusha ngumi wakati sisi tukizungusha gurudumu la Maendeleo ya Taifa, wakati wao wakinyoosha vidole sisi tupambane kunyoosha nidhamu ya Nchi na hasa kwa watumishi na Viongozi wetu.

Ukombozi wa Kiuchumi ni Sera ya CCM Awamu ya V na ni hakika

Ndg. John Pombe Joseph Magufuli watanzania wamekuamini simamia haki zao, unaacha alama kubwa katika maisha ya wananchi wa kawaida, utabarikiwa hapa duniani na mbinguni, komaa baba, sisi watu wa kawaida tuko nawe na tunaona matunda ya kazi zako.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

No comments:

Post a Comment