Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo alipokutana na ujumbe
wa Tume ya Utumishi wa Walimu ulipotembelea Wilaya hiyo mapema leo
ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi. Devotha
Gabriel.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa
Bw. Audiphace Mushi akieleza jinsi uwepo wa Ofisi za Tume ya Utumishi wa
Walimu Wilayani humo ilivyoongeza tija katika kutoa huduma kwa walimu
wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu ulipotembelea Wilaya hiyo
mapema leo.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka
Tume ya Utumishi wa Walimu akimuonesha Katibu Msaidizi wa Tume ya
Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Bw. Edward Chamwela
namna ya kutumia mfumo rasmi wa barua pepe za Serikali (GMS) ili
kuimarisha Mawasiliano ngazi ya Wilaya na Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi akiagana na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA
wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel mara baada ya
kumtembelea Ofisini kwake leo Wilayani Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja
na ujumbe wa Tume ya Utumishi wa walimu mara baada ya kumtembelea
Ofisini kwake mapema leo ukiongozwa na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa
Tume hiyo Bi Devotha Gabriel .
Frank Mvungi- Maelezo – Dodoma
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)
imetajwa kuwa kiungo muhimu katika kuwawezesha walimu kutoa mchango wao
utakaosaidia kukuza Kiwango cha elimu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa ziara ya
Ujumbe wa Tume hiyo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma Mkuu wa Wilaya hiyo
Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa anaipongeza Tume hiyo kwa kuweka
mkazo katika matumizi ya TEHAMA.
“Teknolojia ni jambo muhimu sana
katika kusaidia kuharakisha maendeleo na kuongeza ufanisi kwa kuondoa
udanganyifu unaoweza kujitokeza katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya
kuwahudumia wananchi “ Alisisitiza Ndejembi
Akifafanua zaidi Mhe. Ndejembi
amesema mifumo ya TEHAMA inayoenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa
sasa ni chachu ya maendeleo hapa nchini.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa
Wilaya hiyo Bw. Audiphace Mushi amesema kuwa Tume imewezesha walimu
kutambua haki na wajibu wao,kusaidia walimu kupata haki zao kwa wakati.
Tume ya utumishi wa Walimu imekuwa
mhimili muhimu katika kuwasimamia walimu hivyo ni vyema kila mdau
akasaidia juhudi za Tume ili kuimarisha utendaji wake.
Tume ya Utumishi wa Walimu
imetembelea Wilaya za Chemba, Bahi, Chamwino,Kondoa, Mpwapwa na Kongwa
ili kujionea hali halisi ya utendaji wa Makatibu Wasaidizi wa Tume ngazi
ya Wilaya hali itakayochochea na kuhamasisha wadau kujitokeza na
Kusaidia Tume kukabiliana na changamoto zinazowakabili walimu kote
nchini.
No comments:
Post a Comment