Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa
maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa wanajadili
kitu walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa
maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wametoa msaada wa
mashuka sabini na tano na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi
1,672,500 katika hospitali ya Tosamaganga iliyopo katika katta ya
kalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya
ikizingatiwa kuwa wengi wao waliwahi kutibiwa hapo wakati wanasoma.
akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi
msaada huo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye
pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma
ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini,
Danford Mbilinyi alisema kuwa walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa
wangi wao walikuwa wanatibiwa katika hospital hiyo wakati wakiwa
masomoni miaka mingi iliyopita.
“Leo hii tunaafya njema kwa ajili
tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa tunaumwa na ilitusaidia kufanya
vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii tupo hapa bila kupata huduma
iliyobora nafikiri wengi wetu tusinge kuwa hapa” alisema Mbilinyi
Mbilinyi alisema kuwa wamechangisha
kidogo walichopata wameamua kununua vifaa hivyo ambavyo wanafikiri
vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo hospitalini hapo.
“Hiki kidogo tu lakini tunajua kwa namna
moja au nyingine vinaweza kuwasaidia wagonjwa na kuwapunguzia mzigo
uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu
sana kipindi tukiwa masomoni katika sekondari ya Tosamaganga” alisema
Mbilinyi
Dr Steven Biginagwa ni daktari bingwa wa
magonjwa ya watoto na mtafiti wa ugonjwa wa malaria alisema kuwa
hospital hiyo iliokoa maisha yake kwa kupata huduma bora kwani alikuwa
na ugonjwa wa utumbo kujifunga lakini madaktari waliokoa maisha yangu
hadi hii leo.
“Mimi nililazwa hapa mwezi wa kwaza na
mwezi wa pili wa masomo nilipata matatizo ya huo ugonjwa lakini
nashukuru mungu kuwawezesha wahudumu wote wa hii hospital kunitibu na
kuokoa maisha yangu hadi leo nipo na afya yangu njema na mfanyakazi
niliajiliwa hivyo bila kuwepo kwa hospital hii sijui leo hii ningekuwa
wapi” alisema Dr Biginagwa
Dr Biginagwa alisema kuwa licha ya
kumaliza masomo yake lakini mitihani mine ya mwisho alifanyia hodini
akiwa amelazwa kutokana na ugonjwa aliokuwa nao na madaktari walimsaidia
kupata huduma bora ndio maana alifanya vizuri mitihani kwenye mitihani
na kufaulu vizuri.
“Kwa miaka yangu vyote miwili nimekuwa
nikishinda sana hapa hospitalini lakini mungu alisaidia nikamaliza
masomo yangu na nafikiri kutokana na hudumu nilikuwa napewa hapa ndio
iliyonipelekea kwenda kusomea udaktari na ndio maana hadi leo hii mimi
ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto” alisema Dr Biginagwa
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa
TASAF Ladslausi Mwamanga aliwaomba wananchi popote walipo hapa nchi
kukumbuka kutoa msaada waote katika hospital ili kuendelea kuboresha
sekta ya afya kwa kuwa serikali bila wadau haiwezi kukamilisha kila kitu
yenyewe.
“Unajua kuwa serikali inamambo mengi
ambayo inayaofanya hivyo kukamilisha kila kitu kwa wakati ni vigumu sana
hivyo sasa sisi wadau tuendelee kuisaidia serikali kwa kile tuchokipata
kutoa msaada kwenye sekta hii ya afya ambayo inachangamoto nyingi sana”
alisema Mwamanga
Naye diwani wa kata ya Kalenga Thobias
Kangalawe aliwashukuru wanafunzi hao waliosoma shule ya Tosamaganga
miaka iliyopita kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Tosamaganga,alisema
kuwa ni nadra sana kuona watu wanakumbuka walikopatia mafanikio na
kutoa msaada kama wenu.
Nyinyi watu wa kipekee kabisa toka
nimekuwa kiongozi siajwahi kuona kundi kubwa lenye kujali wapi walikotoa
na kuendelea kutafuta njia mbdala za kusiadia kutatua changamoto kama
nyinyi hivyo hongeni na namuomba mungu awaongezee pale mlipo punguza”
alisema kangalawe
No comments:
Post a Comment