Friday, October 20, 2017

MHE AWESO ATINGA MKOANI MBEYA KUFANYA UKAGUZI WA MIRADI NA VYANZO VYA MAJI

Na Ramadhani Shabani

Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Bukheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Wa Majukumu Yako Yanayoenenda Na Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Ilani Ya Uchaguzi Ya Mwaka 2015/2020 Isememayo Hapa Kazi Tu!

Ikiwa Ni Kawaida Yetu Kukuletea Taarifa Ya Matukio Mbalimbali Yanayofanywa Na Viongozi Wetu Wakiwa Ktk Utekelezaji Wa Majukumu Yao Ya Kikazi Huku Wakiongozwa Na Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu Basi Leo Ndugu Mtanzania Nimekuletea Taarifa Inayomuhusu Mhe Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Ndugu Jumaa Hamidu Aweso.

Ndugu Mtanzania Ikiwa Ni Siku Kadhaa Zimepita Tangia Mhe Rais John Pombe Magufuli Amuamini Na Kumteua Ndugu Jumaa Hamidu Aweso Kuwa Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Ndugu Jumaa Hamidu Aweso Hajawahi Kukaa Ofisini Kwake Kwani Muda Mingi Sana Anautumia Kukagua Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji Ktk Nchi Yetu Ikiwa Ni Pamoja Na Kukagua Na Vyanzo Vya Maji Pia Na Kama Haitoshi Kusikiliza Kero Za Wadau Wakubwa Wa Maji Ambao Ni Wananchi,Ambapo Taarifa Hii Ya Leo Inatufikisha Moja Kwa Moja Wilayani Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.

Mhe Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Ndugu Jumaa Hamidu Aweso Jana 20/10/2017 Amefanya Ziara Ya Ukaguzi Wa Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji Na Vyanzo Vyake Pamoja Na Kusikiliza Kero Za Wadau Mbali Mbali Wa Maji Ambao Ni Wananchi Wilayani Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.

Mhe Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Ndugu Jumaa Hamidu Aweso Akiwa Wilayani Mbeya Vijijini Amekagua Miradi Mikubwa Ambayo Imekamilika Na Ambayo Bado Pia Haijakamilika Ikiwa Ni Utekelezaji Wa Ilani Ya Uchaguzi Ya CCM Ya 2015/2020 Isemayo Hapa Kazi Tu!Huku Malengo Makubwa Ikiwa Ni Kufikia Mahitaji Ya Wadau Wa Kubwa Wa Maji Ambao Ni Wananchi Wetu.

Ndugu Jumaa Hamidu Aweso Ambaye Ndiye Naibu Waziri Mwenye Dhamana Ya Maswala Ya Maji Na Umwagiliaji Hapo Jana Wakati Akiasikiliza Na Kujibia Kero Za Wadau Wakuu Wa Maswala Ya Huduma Za Maji Ambao Ni Wananchi Wetu Wilayani Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya  Aliwasihi Sana Sambamba Na Kuwalingania Wananchi Hao Kutunza Vyanzo Vyote Vya Maji Vinavyopatukana Ktk Mazingira Yanayowazunguka,Huku Akiwa Waonya Wananchi Hao Kuacha Kufanya Shughuli Zao Za Utafutaji Riziki Pembezoni Au Karubi Na Vyanzo Hivyo Vya Maji Huku Akisema Kwamba Vitendo Hivyo Havitavumiliwa Kwani Vimelenga Kuharibu Vyanzo Hivyo Na Kuifanya Serikali Kushindwa Na Kukwama Kuwafikishia Wananchi Wake Huduma Bora Na Stahiki Kulingana Na Mahitaji Yao Ya Maji.

Mhe Naibu Waziri Pia Kama Haitoshi Alipata Fursa Ya Kusikiliza Kero Mbalimbali Zinazo Wakabiri Wananchi Na Haswa Ktk Uboreshaji Wa Huduma Ya Upatikanaji Wa Maji Safi Na Salama Kwa Ajili Ya Matumizi Yao.

Mhe Naibu Waziri Jumaa Hamidu Aweso Alijitahidi Sana Kuzipatia Majibu Na Kuzitatua Moja Kwa Moja Kero Mbalimbali Zilizokuwa Zimewasilishwa Mbele Yake Na Wananchi Wa Wilaya Ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya,Huku Kero Nyingine Akiwa Amazichukua Na Kuahidi Kuzifanyia Kazi Na Kuzipatia Utatuzi Pia.

Tanzania Mpya Si Ndoto Tena Bali Ni Uhalisia Uliolenga Kuendelea Kuijenga Nchi Yetu Ktk Desturi Na Misingi Ya Uchapakazi,Uadilifu Sambamba Na Uzalendo Kwa Kufanya Kazi Kwa Bidii Ktk Kuboresha Maisha Ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment