Kamishna
wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Dk Roselyn
Akombe ametangaza kujiuzulu nafasi yake katika tume hiyo.
Dk
Akombe ametuma taarifa ya kujiuzulu akiwa mjini New York nchini
Marekani anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa
kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika
taarifa yake, Akombe amesema kwamba uchaguzi wa marudio wa uraisi
uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu haujafikia vigezo vya kuwa
uchaguzi huru na wa haki.
Akombe
anajiondoa kwenye tume hiyo ya IEBC ikiwa imebaki wiki moja uchaguzi wa
urais kurudiwa kutokana na matokeo ya awali kufutwa na mahakama kuu na
kuamuru uchaguzi mpya ufanyike.
Agosti Akombe alizuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa JKIA akielekea nchini Marekani.
Dk
Roselyn Akombe Kwamboka alizaliwa 1976 katika kaunti ya Nyamira , na
kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuelekea nchini Marekani
kwa masomo zaidi.
Ana
shahada ya uzamifu katika masuala ya sayansi na kimataifa mbali na
shahada nyengine kama hiyo katika somo hilo kutoka chuo kikuu cha
Rutgers .
Hadi
uteuzi wake katika tume hiyo alifanya kazi kama katibu katika Umoja wa
Mataifa mjini New York, wadhfa ambao anasema ulimwezesha kuwa na uzoefu
katika maswala
Uwezo
wake mkuu amesema mbele ya kamati ya bunge nchini Kenya, ni kutatua
migogoro na kwamba ameishi ng'ambo kwa takriban miaka 15, hatua
iliomwezesha kuelewa zaidi mahitaji ya watu wanaoishi ughaibuni wakati
wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment