Saturday, October 21, 2017

DC MWERA AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE BUSEGA

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Mhe Tano Mwera azindua jukwaa la wanawake Busega.

Mhe Mwera amewataka wanawake kutojibweteka kuelekea uchumi wa viwanda.

Umewataka wanawake kuwa wamiliki wa viwanda na si wafanyakazi tu katika viwanda.

Kwa asili mila na desturi zinamkandamiza mwanamke kama vile kutomiliki ardhi, kutokuwa na maamuzi katika ngazi ya familia, zote hizi zikichagizwa na mfumo dume.

Changamoto zingine ni kama vile ndoa na mimba za utotoni, ukosefu wa taarifa na maalifa, ukatili wa kijinsia na kadhalika.

Ingawa asilimia 71% ya wakulima ni wanawake bado uchumi wao umeendelea kuwa wa chini.

Umewataka wanawake kujipanga kiuchumi, kuwalinda watoto wao ili kuzuia mimba za utotoni ambalo ni janga la Taifa kwa sasa, kupanga uzazi, na kutumia fursa ya asilimia 5 ya pato la halimashauri kuwawezesha kuinua miradi yao katika vikundi vyao.

No comments:

Post a Comment