Sunday, October 8, 2017

CCM IKUNGI WACHAGUA VIONGOZI WAPYA, LIKAPAKAPA KUHUDUMU UENYEKITI KWA MIAKA MITANO

Mwenyekiti mpya wa CCM Ndg Mika Likapakapa akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida wakati akiomba kura kwa wajumbe kabla ya uchaguzi kufanyika.Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kulia) akiteta Jambo na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi mara Baada ya uchaguzi kumalizika.Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitafakari jambo kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida wakifatilia kwa makini mkutano wakati wagombea wa nafasi mbalimbali walipokuwa wakieleza kile watakachokifanya mara Baada ya kuchaguliwa.Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida wakifatilia kwa makini mkutano wakati wagombea wa nafasi mbalimbali walipokuwa wakieleza kile watakachokifanya mara Baada ya kuchaguliwa.Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ikungi wakijiuzulu nafasi zao mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya hiyo.Mwenyekiti mstaafu wa CCM Wilaya ya Ikungi Ndg Hassan Tati akizungumza kabla ya kujiuzulu nafasi yake mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi.Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Ndg Philip Elieza alitoa maelekezo ya namna ya upigaji kura kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya hiyo.Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi akipiga kura wakati wa Mkutano huo.

Na Mathias Canal, Singida

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida wamefanya maamuzi ya kuchagua viongozi katika ngazi mbalimbali watakaohudumu katika kipindi Cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.

Mkutano Mkuu huo wa Wilaya ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali za ndani ya CCM zinazoendelea kote Nchini ulihudhuriwa na jumla ya wajumbe 1034 kutoka kata zote Ishirini na nane za Wilaya ya Ikungi.

Katika Mkutano huo asilimia kubwa ya Wajumbe waliamua Kumchangua Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi ambaye ni Ndg Mika Lucas Likapakapa kwa jumla ya kura 761 huku akiwaacha kwa mbali washindani wake ambao Ni Gwae Naftari aliyepata kura 181 na Juma Sungi aliyepata kura 52.

Katika nafasi mbili za Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu anaibuka kidedea kwa kupata kura 989 ambazo Ni kura nyingi kuliko kiongozi mwingine yeyote aliyezipata katika Uchaguzi huo, mshiindi mwingine katika nafasi hiyo Ni Mhe Mwanga Ally Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa waliochaguliwa Ni Abdallah Aisha Selemani aliyepata kura 815, na Mbugha Mathew Ng'imba aliyepata kura 620. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya walioshinda ni Hambu Shabani Dude aliyepata kura 980, Katanga Jonas Robert aliyepata kura 720, Mghanga Theotini Sirilo ambaye amepata kura 710 na Ntandu Juma Athumani aliyepata kura 703.

Akizungumza mara Baada kutangaza washindi wa nafasi zote, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo Mhe James John Mkwega ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Mwenyekiti ALAT Mkoa wa Singida aliwapongeza Viongozi wote wa Chama Wilaya ya Ikungi kwa kazi kubwa ya kuandaa na kufanikisha uchaguzi huo.

Alisema kuwa ana Imani kubwa kuwa  wajumbe wa Mkutano Mkuu wamechagua viongozi waadilifu, wachapa kazi, wanaochukizwa na Rushwa, wanaopenda watu zaidi kuliko wanavyojipenda wao.

Katika Nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya kundi la wanawake walioshinda ni Makula Fatuma Said aliyepata kura 971, na Mbiaji Fridian Yusuph aliyepata kura 950. Katika nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri Wilaya kundi la Wazazi washindi Ni Andalu Andrea Ntandu kura 980 na Alhaji Chima Salum Mohamed kura 920.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi Mbunge wa Jimbo Hilo Mhe Elibariki Kingu aliwapongeza wagombea wa nafasi zote walioshinda na wale ambao kura zao hazikutosha huku akimsihi Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Ikungi kuunganisha makundi ya wanachama wote ili kuwa na kauli Moja ya kusimamia ilani ya CCM.

Alisema kuwa ana matarajio makubwa kwa viongozi hao waliochaguliwa kuwa watawajibika ipasavyo na kuisaidia serikali inayoongozwa na Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe John Pombe Joseph Magufuli kutekeleza ahadi alizoziahidi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.

Ndg Fransis Sankha ndiye aliyekuwa mshindi katika Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi kwa kupata kura 74 akifuatiwa na Hamisi Yusuph Athumani aliyepata kura 55. Washindi wa Nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya kundi la Vijana Ni Komba Ombeni Hadarian kura 969 na Mughenyi John Mathias kura 902.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa  CCM Wilaya ya Ikungi Ndg Mika Lucas Likapakapa aliwashukuru Wajumbe wote kwa kumpigia kura nyingi ambazo zimetoa ishara ya upendo mkubwa kwake. Aliwasisitiza Wajumbe wote kuwa  Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wanachama wote ni lazima wapaze sauti zao kukemea uovu, Rushwa, Uonevu wa aina yoyote ndani ya Chama na serikali.

Alisema Chama Cha Mapinduzi( CCM) kitaendelea kuwa Chama bora kwa Itikadi,  Muundo, Utendaji, Idadi kubwa ya Wanachama hai ambao mpaka sasa kina jumla ya wanachama wanaokadiriwa Milioni 14,  kwa Afrika kikifuatiwa na ANC cha Afrika ya Kusini na kikishika nafasi ya Pili Duniani kikiongozwa na Chama cha Kikomunisti cha watu wa Uchina.

CCM ipo katika hatua za mwisho za kupata wawakilishi wote katika ngazi za Wilaya ikiwa ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali zinazoendelea Nchi nzima zilizoanzia ngazi ya Mashina mpaka itakapofikia ukomo katika ngazi ya Taifa mwezi Novemba Mwaka huu.

MWISHO

No comments:

Post a Comment